Matukio : Waliokaidi kuhama kwenye maeneo yenye mafuriko sasa kukamatwa - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Thursday, 31 May 2018

demo-image

Matukio : Waliokaidi kuhama kwenye maeneo yenye mafuriko sasa kukamatwa


_MG_8122 Eneo la Kitongoji cha Mferejini lililotengwa na Serikali kwa ajili ya kuanzisha kambi kwa ajili ya Wahanga wa Mafuriko .

_MG_8128 Wahanga wa Mafuriko wakianza ujenzi wa nyumba za Miti kwa ajili ya kujisitiri katika eneo la Ruvu Mferejini.

_MG_8134

_MG_8152 Makazi ya wananchi hawa kwa sasa wanalala nje ,wakiteseka na Baridi,Mbu na wanyama wakali kama Nyoka hali ambayo inatishia Afya zao.

_MG_8141 Hata hivyo tayari serikali imeanza kufikisha huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo ya Maji kwa ajili ya kunywa pamoja na kupikia.

_MG_8153

_MG_8124 Na hizi ndio sehemu za makazi ya wananchi hawa.

_MG_8160

_MG_8169 Huduma Muhimu kama Choo zimeanza kujengwa katika eneo hilo.

_MG_8250 Wananchi Jamii ya Massai pia ni miongoni mwa waathirika wa Mafuriko hayo.

_MG_8253

_MG_8256

_MG_8262 Mkuu wa wilaya ya Same,Rosemery Senyamule akiwa ameongozana na Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro,Mhandisi Aisha Amour wakitembelea moja ya Kaya ya Jamii ya Wafugaji walioanza maisha mapya katika maeneo yaliyotengwa na Serikali.

_MG_8270

_MG_8275 Baadhi ya Nyumba za Jamii ya Kimasai zikianza kujengwa katika eneo hilo.

_MG_8284 Kama ilivyo ada kwa tamaduni za Mila za jamii ya Maasai kina mama ndio watendaji wakubwa wa shughuli za Nyumbani kiwemo ujenzi wa Nyumba kama anavyoonekana Bibi huyu.

_MG_8281 Arikadharika shughuli ya uchotji wa maji vivyo hivyo.

_MG_8295 Na hii ni Familia moja ya Fashet Kimotong wakiwa katika eneo jipya baada ya kuhama makazi yao ya wali kufuatiwa Nyumba zao kuzingirwa na maji .



Na Dixon Busagaga ,Kanda ya Kaskazini.


SERIKALI imetoa siku mbili kwa wananchi waliosalia katika Vijiji vya Ruvu Mferejini na Ruvu Marwa wilayani Same ,Mkoani Kilimanjaro vilivyozingirwa na maji kuondoka mara moja na kwamba watakao kaidi wataondolewa kwa kutumia nguvu na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.


Zaidi ya watu wapatao 2000 wamelazimika kuyahama makazi yao baada ya kufikwa mafuriko kutokana na mvua kubwa za masika zinazoendelea kunyesha huku eneo lililoathirika zaidi na mvua hizo ni ukanda wa tambarare wa wilaya ya Same unaopakana na Bwawa la Nyumba ya Mungu.





Licha ya Idadi hiyo ya watu kuyahama makazi yao lakini bado wapo waliokaidi kuondokana na hapa Serikali kupitia Mkuu wa wilaya ya Same ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya Wilaya hiyo ,Rosemerry Senyamule ,ikatoa agizo.


Serikali imetenga maeneo kando ya milima iliyopo katika kitongoji cha Mferejini kwa ajili ya Kambi za Muda kwa watu waliokosa Makazi ,Clouds Habari imefika katika Kambi hizo na kujionea maisha mapya ya wahanga wa mafuriko huku misaada ya kibinadamu ikihitajika zaidi .

Licha ya kukosekana kwa baadhi ya huduma katika eneo hili bado wananchi hawa wanahitaji msaada wa hali na mali ili angalau kuweza kunusuru Maisha yao kutokana na Baridi kali ,Mbu na hata wanyama wakali wakiwemo Nyoka.

Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi ,Aisha Amour ni miongoni mwa baadhi ya viongozi waliowatembelea wahanga wa mafuriko kwa ajili ya kutoa pole .

Mafuriko katika vijiji hivi yanatajwa kuwa hutokea kila baada ya Miaka 10 na kwamba mara ya mwisho yalitokea mwaka 2008 huku chanzo kikitajwa kuwa ni kujaa kwa Bwawa la Nyumba ya Mungu ambapo ujazo ulifikia Mita za ujazo 689.88 ambazo kwa sasa zimeanza kupungua hadi kufikia mita za ujazo 689.80 baada ya maji kuanza kuelekea kwenye maeneo ya makazi kwa kupitia mto Pangani.

No comments:

Post a Comment

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *