Matukio : Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge watembelea mradi wa ILMIS na Majengo ya NHC Victoria na Morocco - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


19 May 2018

Matukio : Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge watembelea mradi wa ILMIS na Majengo ya NHC Victoria na Morocco



Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akionyesha Faili lenye viambatanisho vya hati moja katika chumba cha kubadilisha hati za kawaida kwenda Dijitali kinachosimamiwa na mradi wa ILMIS, ambapo kwa sasa mtu ataweza kupata hati yake kupita mtandao na akihitaji karatasi atapata moja amabyo itakuwa na viambatanisho vyote.

Msajili wa Hati kutoka Wizara ya Ardhi, Joanitha Kazinja akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Maliasili, Nape Nnauye wakati walipotembelea chumba cha kubadilishia Nyaraka cha Mradi wa ILMIS.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Maliasili, Nape Nnauye Akizungumza wakati wa kikao cha Majumuisho ya ziara ya kutmebelea Miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Mradi wa ILMIS Unaotekelezwa na Wizara ya Ardhi.

Mtaalamu wa Maluala ya bacode Katika mradi wa ILMIS Cristina Selaru akitoa maelezo kwa Kamati ya kudumu ya Bunge Ardhi na Maliasili jinsi mfumo huo utakavyokuw aunafanya kazi kumsaidia mtu kujua taharifa zake zote.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi na Maliasili na Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Njombe, Neema Mgaya akitizama jinsi wafanyakazi wa Mradi wa ELMIS wakijaza baadhi ya nyarak katika mtandao.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Maliasili, Nape Nnauye akizungumza jambo na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi mara baada ya kutembelea mradi wa Victoria unaotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Maliasili, Nape Nnauyeakiongoza kikao cha Kamati.

Mkurugenzi wa Mfumo wa TEHAMA Wizara ya Ardhi na Kodineta wa ILMIS , Dk Shabani Pazi Akitoa Maelezo juu mradi huo.

Mhandisi Msimamizi wa Mradi wa ILMIS,Carol Roffer akieleza jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge walipotembelea kuona mafanikio ya Mradi huo unatoekelzwa na Wizara ya Ardhi.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge wakipanda kwenye gari kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa NHC.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad