MKUU wa wilaya ya Lushoto January Lugangika akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani cha Halmashauri ya Bumbuli ambacho kwa mara ya kwanza kilifanyika eneo la makao makuu ya Kwehangara
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bumbuli Peter Nyalali akizungumza katika kikao cha robo ya mwaka cha Baraza la Madiwani kilichofanyika eneo Jipya la Makao Makuu ya Halamshauri hiyo Kwehangala kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Amiri Sheiza
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bumbuli Amiri Sheiza akizungumza katika kikao hicho kwa kuwataka wananchi kuwa wamoja kuhakikisha halmashauri hiyo inbapata mafanikio kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauti ya Bumbuli Peter Nyalali
Mkurugenzi wa Halmashauti ya Bumbuli Peter Nyalali kushoto akiwa na Mwenyekiti wa Halma shauri ya Bumbuli Amiri Sheiza wakifuatilia hoja mbalimbali kwenye kikao hicho
Mkuu wa wilaya ya Lushoto January Lugangika kulia akipitia makabrasha kwenye kikao hicho
Sehemu ya madiwani wakifuatilia kikao hicho
Sehemu ya wananchi waliopata fursa ya kuhudhuria baraza hilo
MKUU wa wilaya ya Lushoto mkoani Tanga January Lugangika amewataka madiwani wa halmshauri ya Bumbuli kuhakikisha wanashiriki katika kukagua miradi inayotekelezwa kwenye maeneo mbalimbali ili kuiepusha kujengwa chini ya kiwango na hivyo kukosa tija kwa wananchi.
Agizo hilo alilitoa juzi wakati akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani cha kawaida cha robo tatu kilichofanyika kwa mara ya kwanza katika makao makuu mapya ya halmashauri hiyo eneo la Kwehangara.
Alisema iwapo madiwani hao watashindwa kukagua miradi hiyo inatoa mwanya kwa wakandarasi kushindwa kuitekeleza kwa viwango vinavyotakiwa hali inayopelekea kukosa tija na thamani halisi ya fedha zinazotumika. “Ndugu zangu madiwani hakikisheni mnakagua miradi ya maendeleo hili ndio jukumu lenu la msingi kwani msipofanya hivyo ndipo wakandarasi wanafanya miradi hiyo isiwe na tija na hivyo matokeo yake gharama inayotumika inakosa thamani yake”Alisema DC Lugangika.
Aidha pia alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Peter Nyalali kuweka utaratibu mzuri kwa madiwani ili waende kukagua miradi inayotekelezwa hususani miradi ya maji ambayo imekuwa ikihujumiwa kutokana na wakandarasi”Alisema.Nay kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bumbuli Amiri Sheiza alisema wanamshukuru Rais John Magufuli kwa kuwasaidia kuwatatulia mambo mawili makubwa kwao kuyapatia ufumbuzi.
Alisema suala la kwanza ni ujenzi wa Jengo la Halmashauri eneo la Kwehangara na pili ni ufunguzi wa kiwanda cha Mponde katika mambo hayo ameonyesha namna anavyotujali.“Hivyo tunamuomba Mungu amuongezee hekima na busara katika kuiendesha nchi na pia napenda kumthibitishia Rais kwamba wananchi, Baraza la Madiwani pamoja na kupishana kifikra bado tupo pamoja kufanya kazi bila kubaguana”Alisema.
Hata hivyo alionya kuwa mtu ambaye ataanzisha vimaneno kuhusu suala hilo watamchukulia hatua kali kwa sababu atakuwa hana nia njema na wananchi wa halmashauri hiyo katika kuwaletea maendeleo.
“Nionyesha mtu yoyote atakayeleta vimaneno kuhusu suala hili sisi hatutamvumilia tutamchukulia hatua kali kwani wana Bumbuli na mbunge wetu sote pamoja “Alisema.
(Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
No comments:
Post a Comment