Matukio : Vijana washauriwa kuwa washiriki wa Maendeleo na sio wanaoyasubiri - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 28 May 2018

Matukio : Vijana washauriwa kuwa washiriki wa Maendeleo na sio wanaoyasubiri





Na Mwandishi wetu
MRATIBU Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez amewataka vijana wa Tanzania kuwa washiriki katika mipango ya maendeleo na sio kusubiri kufanyiwa.


Aidha ameshauri vijana kuacha kuilalamikia serikali na jumuiya ya kimataifa kuhusu ajira na badala yake wajiulize wamelifanyia nini taifa na jumuiya hiyo.


Alisema katika kipindi ambacho theluthi mbili ya watu nchini ni vijana, wasitarajie kuajiriwa au kupatiwa kazi kirahisi kwa kuwa idadi ni kubwa kuliko hata yeye alipokuwa akisoma.


Alisema tatizo la ajira kwa sasa haliwezi kusubiri serikali au wahisani ni tatizo linalokuwa kibinafsi zaidi na kuhitaji vijana katika uwingi wao kuamka na kubuni vitu vitakavyoleta maendeleo yao binafsi na pia ya kitaifa.


Akizungumza katika jukwaa la vijana la AIESEC mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Dar es salaam Mratibu huyo alisema kwamba vijana wanatakiwa kushiriki katika kila kitu na kuacha kushutumu serikali au jumuiya ya kimataifa katika kipindi ambacho dunia imebarikiwa na vijana kama nguvu kazi yake kubwa.


Aliwataka vijana kujadili kuhusu malengo ya dunia, fursa zake, utekelezaji wake na changamoto zake.


“Malengo ya Dunia ni ajenga muhimu sana kwa Tanzania, Afrika na ulimwenguni kote. Ajenda hii imelenga kuleta mabadiliko chanya kwa kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma katika utekelezaji wake” alisema Alvaro na kuongeza kuwa malengo hayo 17 ni lazima yajulikane ili kil kijana ashiriki katika utekelezaji wake.


Alisema vijana wakiwa ndio viongozi wa baadae ni lazima waelewe malengo hayo ya dunia na namna ya kuyatekeleza kwa kuyafungamanisha na mpango wa maendeleo wa miaka mitano wa taifa.


Alisema kwa vijana kuangalia na kutambua wataweza pia kuona ni kwa namna gani wao ni watekelezaji wa malengo hayo na wala si wasindikizaji.


Aidha aliwataka wakiwa kama vijana wanatakiwa kuwa wbaunifu katika eneo walilipoo na kuhakikisha kwamba linapata mafanikio makubwa.


“Kwa wale wanaonifuatilia katika twita mtakumbuka niliposti habari za kijana wa miaka kumi na minane ambaye alitengeneza mkono wa roboti unaofanyakazi kutoka katika mabaki ya vifaa vya matumizi ya nyumbani. Huu ndio ubunifu tunaoutaka, wa kutambua changamoto na suluhu zake” alisema Alavaro katika jukwaa hilo lililofanyika Makumbusho jijini Dar es salaam.


Alisema anaamini kuwa Mpango wa dunia wa maendeleo endelevu sio Biblia wala Kurani na kuwataka vijana kuuangalia, kuutafakari kuujadili na kujua namna ya kuendesha utekelezaji wake kwani imebaki miaka 12 kumalizika kwa utekelezaji.


Alisema ili kufikia adhima ya kuutokomeza umaskini ifikapo mwaka 2030 ni vyema vijana wakatumia wakati kwa makini kuangalia malengo hayo 17 na kuona namna ya wao kuwa washirika.


Aidha katika hotuba yake hiyo alihimiza vijana kufanya mambo kwa wakati:” Vijana tufanye ya wakati, wakati tuna wakati, kwani utafikia wakati tunataka kufanya ya wakati, wakati hatuna wakati”


Akizungumzia nguvu ya mtandao , Alvaro aliwataka vijana kuwa smati katika kuchagua mambo yanayofaa kwa maendeleo yao na sio kuchukua mambo ambayo yatawaangamiza au kuleta vurugu.


Katika jukwaa hilo ambalo liliongozwa na Mratibu huyo kulikuwa na wasemaji wengine wakiwemo Rais wa AIESEC Tanzania, Amani Shayo; Mkurugenzi Mkazi wa Trade Mark East Africa, John Ulanga na Mkurugenzi Mtendaji wa Empower, Miranda Naiman wote hao waliwataka vijana kuwa sehemu ya mafanikio.


Mmoja wa wa shiriki Debora Kaluzi kutoka Chuo cha Diplomasia ambaye pia ni championi wa malengo endelevu ya dunia alisema kama champion amefarijika kuwepo katika jukwaa hilo kujadili mambo mbalimbali yanayosukuma maendeleo ya nchi na vijana.


Alisema akiwa championi yeye anajikita zaidi katika lengo la nne na la tano ambalo linahakikisha kwamba wasichana wanakuwa na uwezo huku wakijua thamani yao katika jamii.


Alisema utekelezaji wa malengo hayo yatasaidia wanawake kujitambua na kufikia lengo la wao kushiriki kikamilifu katika masuala yanayohusu mambo mbalimbali ya kidunia yakiwemo ujasirimali na madaraka.


Alisema wanawake wakipewa fursa na kukawepo na haki sawa ya jinsia wanaweza kubadilisha mambo mbalimbali yanayohusu dunia wanayoishi.


Naye Amani Shayo katika mahojiano pamoja na kuzungumza na vijana alisema kwamba akiwa Rais wa AIESEC, Shirika la vijana lililoanzishwa mwaka 2000 Chuo Kikuu kwa lengo la kuwasaidia vijana kujitambua katika masuala ya uongozi, anaamini kwamba jukwaa ni sehemu kubwa ya kufanikisha vijana kujitambua na kujiipanga kushiriki maisha yanayotakiwa katika jamii.


Alisema kupitia kazi za kujitolea vijana wanazungumza kuhusu malengo ya maendeleo endelevu 17 yaliyopangwa na dunia na kuhakikisha kwamba wanafanikisha adhima ya dunia.


Alisema utafiti uliofanywa kwa takaribani vijana 2000 umewapa wazo la nini wanatakiwa kufanya na moja ya mambo ambayo yalijadiliwa katika Jukwaa ni namna ambavyo vijana wanaweza kuwezeshwa kujiajiri kuajiriwa na pia kushiriki kikamilifu katika miradi mbalimbali ya utoaji huduma na kadhalika.


Alisema shirika hilo lina mradi wa kuwezesha vijana kushiriki katika kazi za kujitolea ndani na nje ya nchi na pia kutoa elimu ya kuongeza ujuzi.


Alisema kazi kubwa ya jukwaa ni kuwaleta pamoja watawala na viongozi na wadau wa maendeleo ambao watashirikiana na vijana kudadavua malengo hayo ya dunia na kuyawezesha kufanyakazi katika maeneo ambapo vijana wenyewe wapo.

Rais wa AIESEC Tanzania, Amani Shayo akizungumza kuhusu AIESEC na kazi zake ambapo alisema jukwaa hilo lengo lake ni kuwasaidia vijana kujitambua katika masuala ya uongozi, anaamini kwamba jukwaa ni sehemu kubwa ya kufanikisha vijana kujitambua na kujiipanga kushiriki maisha yanayotakiwa katika jamii wakati wa jukwaa la vijana la AIESEC lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.

Mgeni rasmi Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na vijana wa kutoka vyuo mbalimbali walioshiriki kwenye jukwaa la vijana la AIESEC lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.

Msimamizi wa mazungumzo ambaye pia ni Mkuu wa Mafunzo na Miradi wa Empower Ltd, Ella Naiman (kushoto) akizungumza na kuwatambulisha wazungumzaji wakati wa jukwaa la vijana la AIESEC lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd. Kutoka kulia ni Allen Kimambo, Miranda Naiman, Mkurugenzi Mkazi wa Trade Mark East Africa, John Ulanga pamoja na Petrider Paul.

Mkurugenzi Mkazi wa Trade Mark East Africa, John Ulanga (katikati) akizungumza kwenye jukwaa la vijana la AIESEC ambapo alisema vijana wanatakiwa kutoa mchango mkubwa katika kuhakikisha nchi inafikia malengo ya maendeleo endelevu ambayo utekelezaji wake unaishia mwaka 2030 wakati wa jukwaa hilo lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.

Mzungumzaji katika jukwaa la vijana la AIESEC, Mkurugenzi Mtendaji wa Empower Ltd, Miranda Naiman (wa pili kulia) akizungumza wakati wa jukwaa hilo lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.

Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL Group, Irene Mutiganzi akiwasilisha mada kuhusu mitandao ya kijamii ambapo alisema matumizi ya mitandao ya kijamii yakitumika sahihi yatasaidia kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) wakati wa jukwaa la vijana la AIESEC lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.

Mshehereshaji wa jukwaa la vijana la AIESEC, Walter Odemba akiendesha shemsha bongo kuhusu uelewa wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa vijana kutoka vyuo mbalimbali walioshiriki jukwaa hilo lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.

Mgeni rasmi Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez akijibu maswali kwa washiriki wa jukwaa la vijana la AIESEC kuhusu malengo ya maendeleo endelevu na umuhimu wa vijana kushiriki moja kwa moja ambalo limefanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.


Baadhi ya vijana kutoka vyuo mbalimbali wakichangia maoni wakati wa jukwaa la vijana la AIESEC lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower.



Baadhi ya vijana kutoka vyuo mbalimbali walioshiriki jukwaa la vijana la AIESEC lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.

Sekretarieti ya maandalizi ya jukwaa la vijana la AIESEC lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.

No comments:

Post a Comment