Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde, akipeana mikono na mama mjane, Atulehemu Kiduko, ambaye analipwa fidia ya kila mwezi kufuatia kifo cha mumewe wakati akiwa kazini kwenye kiwanda cha karatasi Mgololo kilichoko Mufindi mjini Iringa. mama huyo alitoa ushuhuda wa huduma anayopata kutoka WCF wakati wa kutano baina ya Serikali na wadau wa Mfuko wa Fidia
kwa Wafanyakazi (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta
Binafsi Tanzania, (TPSF) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo
(TCCIA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini uliofanyika jijini Mbeya Mei 26, 2018 kwa lengo la kujadiliana namna bora zaidi
ya utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF Bw. Masha Mshomba.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde, akifungua mkutano baina ya Serikali na wadau wa Mfuko wa Fidia
kwa Wafanyakazi (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta
Binafsi Tanzania, (TPSF) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo
(TCCIA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini uliofanyika jijinmi Mneya Mei 26, 2018 kwa lengo la kujadiliana namna bora zaidi
ya utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mbeya
SERIKALI
ilianzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa lengo la kuhakikisha kuwa
wafanyakazi wanapata mafao bora na stahiki ya fidia tofauti na sheria ya zamani
iliyotoa viwango vya chini vya fidia, lakini pia kuwawezesha waajiri
kupata muda zaidi kushughulikia masuala yao ya uzalishaji na uendeshaji.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia
masuala ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde, jijini Mbeya leo Mei
26, 2018 wakati akifungua mkutano baina ya Serikali na wadau wa Mfuko wa Fidia
kwa Wafanyakazi (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta
Binafsi Tanzania, (TPSF) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo
(TCCIA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kwa lengo la kujadiliana namna bora zaidi
ya utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi.
Mhe.
Mvunde alisema viwango vya juu vya malipo ya fidia kwa wafanyakazi walipokuwa
wanaumia kazini kabla ya sheria ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, ilikuwa ni
shilingi 108,000/=kwa mfanyakazi aliyepata ajali au kuumia kazini, lakini pia
sheria inasema kulikuwa na malipo mengine ya shilingi 83,000/= kwa mfanyakzi
aliyefariki kwa ajali au ugonjwa kutokana na kazi aliyokuwa akifanya na malipo
hayo yalitegemea pia mkataba wa ajira yake unasemaje.
“Serikali
ilikuja na sheria mpya baada ya kuona viwango hivi kwa ubinadamu na kwa hali
halisi, vilikuwa vimepitwa sana na wakati na wafanyakazi walikuwa wanapata
fidia hiyo kwa kadhia kubwa sana na viwango hivyo haviendani na ukuaji wa
uchumi na kwa wakati tulionao.” Alifafanua Mhe. Naibu Waziri.
Aidha
Mhe. Mavunde alisema, Mfuko unafaida kubwa sio tu kwa wafanyakazi bali pia kwa
waajiri na taifa kwa ujumla ambapo wafanyakazi sasa wanauhakika wa kupata
kinga ya kipato kutoakana na majanga ambayo yatasababishwa na ajali, magonjwa
ama vifo kutokana na kazi wanazofanya, lakini waajiri nao watapata muda zaidi
wa kushughulikia masuala yao ya uzalishaji na uendelevu wa biashara na shughuli
zao kwani Serikali kupitia Mfuko itabeba mzigo wote wa gharama pindi
mfanyakazi atakapofikwa na janga lolote awapo kazini.
“Pamoja
na uchanga wake, Mfuko huu ambao umeanzishwa mwaka 2015 umeonyesha mafanikio
makubwa katika kipindi kifupi kwani hadi sasa waajiri ambao wameshajisajili
kwenye mfuko wetu ni 13,500 na wafanyakazi wao ambao wamepatwa na majanga
wakiwa kazini wameshalipwa fidia na Mfuko fedha zisizopungua shilingi bilioni
2.52 kufikia Februari 2018.” Alibainisha.
Alisema
Mfuko umekuja wakati muafaka kwani nchi inakwenda kwenye uchumi wa viwanda bila
shaka kutakuwepo na ongezeko la ajali na magonjwa yanayotokana na uendeshaji wa
shughuli katika viuwanda vyetu hivyo ni lazima kiwepo chombo kitakachosimamia
majukumu haya ya fidia ili kuwapa nafasi pana waajiri kuendelea na shughuli zao
za uzalishaji.
“Rais
wetu wa Jamhuri ya uungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli kila wakati
tunapokutana kwenye baraza la Wafanyabiashara Tanzania amekuwa akituagiza sisi
wasaidizi wake, kama kuna jambo lolote linajitokeza na sekta binafsi inafikiri
kwamba jambo hili bado halijaeleweka na haliko sawasawa ni wajibu wetu sisi
mawaziri kuchukua hatua haraka za kukutana na kujadiliana na wadau na kushauriana
na wadau husika ili kufikia muafaka na kuelewana ili kwenda pamoja na ndio
maana leo tuko hapa.” Alifafanua Mhe. Naibu Waziri Mavunde
Wakitoa
ushuhuda mbele ya washiriki wa mkutano huo, Wafanyakazi waliopatwa na majanga
ya kuumia au kufiwa na wenza wao, wameipongeza Serikali kwa kuanzisha Mfuko huo
kwani umekuwa ni mkombozi kwa wafanyakazi.
“Mimi
nilikatika vidole vya mkono wangu wa kushoto wakati nikitekeleza majukumu yangu
ya kazi kwenye kiwanda cha Lake Cement kinachozalisha saruji ya nyati (Nyati
cement) huko Kimbiji jijini Dar es Salaam na WCF imenilipa fidia ya mkupuo ya
kiasi cha shilinhgi milioni 11, alisema Bw. Jimmy Samson Malumbo mbele ya
Mkutano huo.
Mwingine
aliyetoa ushuhuda wa faida ya Mfuko kwa wafanyakazi, ni mama mjane, Bi. Atulehemu
Kiduko wa huko Mafinga Mkoani Iringa, alisema mumewe ambaye alikuwa mfanyakazi
wa kiwanda cha karatasi Mgololo Mufindi Papers baada ya kuangukiwa na gogo
wakati akitekeleza majukumu yake. Hivi sasa mama huyo mjane anapokea malipo ya
fidia kila mwezi shilingi 110,000/= na watoto wake wawili kila mmoja analipwa
shilingi 55,000/= kila mwezi.
“Kwakweli
nimefarijika sana kwa malipo haya, ingawa nimeshampoteza mwenzangu, lakini
fidia hii ninayolipwa imekuwa ikinisaidia sana katika kuhudumia familia yangu kijijini
ikiwa ni pamoja na kumsomesha motto wangu
mmoja aliye darasa la tatu.” Alisema Bi. Atulehemu.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba
alisema Mfuko unaendeshwa kwa msingi wa utatu ambapo katika bodi ya wadhamini
ambayo ina uwakishi wa serikali, wafanyakazi na uwakilishi wa waajiri kama
ambavyo Shirika la Kazi Duniani linavyotaka katika masuala haya ya fidia kwa
wafanyakazi.
Alisema,
katika mfumo wa zamani, mfanyakazi anapotoka au kwenda kazini endapo atapatwa
na tatizo njiani sheria ya zamani haikumtambua, tofauti na sheria ya sasa
ambapo inaeleza mfanyaakzi akiumia au akifikwa na umauti wakati akitoka kazini
au akielekea kazini sheria ya sasa inataka afidiwe.
“Alisema
Mfuko umeweka utaratibu ili kuhakikisha mfumo wa usajili wa waajiri unakuwa wa
haraka na rahisi lakini pia kushughulikia masuala ya ulipaji fidia katika
kipindi kifupi.” Alisema.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba akizungumza. |
Sehemu ya waliohudhuria mkutano huo.
Sehemu ya waliohudhuria mkutano huo.
Sehemu ya waliohudhuria mkutano huo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji, wa WCF, Bw. Anselkim Peter, akiwasilisha mada kuhusu shughuli za Mfuko.
Mkurugenzi wa huduma za Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, akitoa mada kuhusu namna tathmini inavyofanyika kwa Mfanyakazi aliyepatwa na madhara wakati akitelekeaza wajibu wake wa kazi.
Mwakilishi kutoka chama cha waajiri Tanzania, (ATE), Bi. Patricia Chao, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mbeya, Dkt. Lwitiko Mwakalukwa, akizungumza kwenye mkutano huo. |
Washiriki wakipiatia taarifa mbalimbali za WCF.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, (kushoto), Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo, Bw. Anselim Peter, (wapili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, Bi. Laura Kunenge, na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalaam Omar, (aliyeipa mgongo camera), wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, WCF, Bi. Laura Kunenge |
Emiliana Gwagilo, Afisa Matekelezo wa WCF, akiandaa taarifa kwenye meza kuu
Afisa Matekelezo wa WCF, Bw. George Faustin, akijibu baadhi ya hoja zilizojitokeza kutoka kwa washiriki wa mkutano.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF , akibadilkishana mawazo na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bw. Anselim Peter, (kulia), Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalaam Omar, (kushoto) na Afisa Matekelezo, Bi. Emiliana Gwagilo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Anselim Peter, (katikati)), Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdulsalaam Omar na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, WCF, Bi. Laura Kunenge, wakiwajibika mwanzoni mwa mkutano huo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Anselim Peter, (kushoto), na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, WCF, Bi. Laura Kunenge, wakiwajibika kwenye mkutano huo.
Naibu waziri Mavunde, akisindikizwa na Bw. Mshomba wakati akiondoka kwenye eneo la mkutano.
No comments:
Post a Comment