Maisha /Afya : Taasisi ya Wanaume Yajitolea kutoa Damu - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

Thursday, 3 May 2018

Maisha /Afya : Taasisi ya Wanaume Yajitolea kutoa Damu



Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanaume ya Men at work Maxwell Stanslaus akizungumza na Mkazi wa Arusha katika zoezi la uchangiaji wa damu lililoendeshwa ma taasisi yake.Picha na Ferdinand Shayo



Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Taasisi isiyokua ya kiserikali ya Wanaume inayojulikana kama Men At Work imeendesha zoezi la kuchangia damu kwa ajili ya kinamama wanaojifungua na kupoteza damu nyingi pamoja majuruhi wanaonusurika na ajali na kufikishwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru .



Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Maxwell Stanslaus amesema kuwa wameamua kuwa wameamua kuchangia damu kama mchango wanaume kujitoa kwa ajili ya jamii na kuisaidia jami kwasababu wanaume ni nguzo ya familia,jamii na taifa kwa ujumla.



Max aliwataka wanaume wote nchini kuwajibika na kuwa mstari wa mbele katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii .


“Kwa sasa tumeamua kushirikiana na kitengo cha damu salama kuchangia damu ili kupunguza changamoto ya upungufu wa damu katika benki ya damu “ Alisema Max



Max alisema kuwa taasisi hiyo ina kazi kuwa ya kuwahasisha wanaume kuwa wawajibikaji na kushiriki katika nafasi za malezi familia na jamii ili kujenga familia imara na hatimaye taifa imara.



Kwa upande wake Mwanachama wa Men At Work Rodgers Nelson alisema kuwa anajisikia faraja kuchangia damu ili kusaidia kuokoa maisha ya kinamama wajawazito ambao hupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.

Naye Shemeji Melayeki alieleza kuwa ni mara yake ya kwanza kutoa damu hivyo amewatoa hofu wananchi kutokua waoga wa kuchangia damu kwani zoezi hilo linafanyika kwa umakini na halina madhara yoyote.

No comments:

Post a Comment