WAZIRI JENISTA MHAGAMA AFUNGUA MKUTANO WA WADAU KUJADILI NAMNA BORA ZAIDI YA UTEKELEZAJI WA SHERIA YA FIDIA KWA WAFANYAKAZI
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, DODOMA
SERIKALI
ilianzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa lengo la kuhakikisha kuwa
wafanyakazi wanapata mafao bora na stahiki ya fidia tofauti na sheria ya zamani
iliyotoa viwango vya chini vya fidia, lakini pia kuwawezesha waajiri kupata muda
zaidi kushughulikia masuala yao ya uzalishaji na uendeshaji.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi , Ajira,
Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama mjini Dodoma mwishoni Aprili 13, 2018, wakati akifungua mkutano wa wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF),
Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF-Tawi
la Dodoma) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA-Tawi la
Dodoma) na Chama cha Waajiri Tanzania, (ATE), kwa lengo la kujadiliana namna bora zaidi ya utekelezaji wa sheria ya
fidia kwa wafanyakazi.
Mhe.
Waziri alisema viwango vya juu vya malipo ya fidia kwa wafanyakazi walipokuwa
wanaumia kazini kabla ya sheria ya kuanzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, ilikuwa
ni shilingi 108,000/=kwa mfanyakazi aliyepata ajali au kuumia kazini, lakini pia
sheria inasema kulikuwa na malipo mengine ya shilingi 83,000/= kwa mfanyakzi
aliyefariki kwa ajali au ugonjwa kutokana na kazi aliyokuwa akifanya na malipo
hayo yalitegemea pia mkataba wa ajira yake unasemaje.
“Serikali
ilikuja na sheria mpya baada ya kuona viwango hivi kwa ubinadamu na kwa hali
halisi, vilikuwa vimepitwa sana na wakati na wafanyakazi walikuwa wanapata
fidia hiyo kwa kadhia kubwa sana na viwango hivyo haviendani na ukuaji wa
uchumi na kwa wakati tulionao.” Alifafanua Mhe. Waziri.
Aidha
Mhe. Waziri alisema, Mfuko unafaida kubwa sio tu kwa wafanyakazi bali pia kwa
waajiri na taifa kwa ujumla ambapo wafanyakazi sasa wanauhakika wa kupata kinga ya
kipato kutoakana na majanga ambayo yatasababishwa na ajali, magonjwa ama vifo
kutokana na kazi wanazofanya, lakini waajiri nao watapata muda zaidi wa
kushughulikia masuala yao ya uzalishaji na uendelevu wa biashara na shughuli zao
kwani Serikali kupitia Mfuko itabeba mzigo wote wa gharama pindi mfanyakazi
atakapofikwa na janga lolote awapo kazini.
“Pamoja
na uchanga wake, Mfuko huu ambao umeanzishwa mwaka 2015 umeonyesha mafanikio
makubwa katika kipindi kifupi kwani hadi sasa waajiri ambao wameshajisajili
kwenye mfuko wetu ni 13,500 na wafanyakazi wao ambao wamepatwa na majanga
wakiwa kazini wameshalipwa fidia na Mfuko fedha zisizopungua shilingi bilioni
2.52 kufikia Februari 2018.” Alibainisha.
Alisema
Mfuko umekuja wakati muafaka kwani nchi inakwenda kwenye uchumi wa viwanda bila
shaka kutakuwepo na ongezeko la ajali na magonjwa yanayotokana na uendeshaji wa
shughuli katika viuwanda vyetu hivyo ni lazima kiwepo chombo kitakachosimamia
majukumu haya ya fidia ili kuwapa nafasi pana waajiri kuendelea na shughuli zao
za uzalishaji.
“Rais
wetu wa Jamhuri ya uungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli kila wakati
tunapokutana kwenye baraza la Wafanyabiashara Tanzania amekuwa akituagiza sisi
wasaidizi wake, kama kuna jambo lolote linajitokeza na sekta binafsi inafikiri
kwamba jambo hili bado halijaeleweka na haliko sawasawa ni wajibu wetu sisi
mawaziri kuchukua hatua haraka za kukutana na kujadiliana na wadau na
kushauriana na wadau husika ili kufikia muafaka na kuelewana ili kwenda pamoja
na ndio maana leo tuko hapa.” Alifafanua Mhe. Waziri Jenista Mhagama.
Wakitoa
ushuhuda mbele ya washiriki wa mkutano huo, Wafanyakazi waliopatwa na majanga
ya kuumia au kufiwa na wenza wao, wameipongeza Serikali kwa kuanzisha Mfuko huo
kwani umekuwa ni mkombozi kwa wafanyakazi.
“Mimi
nilikatika mkono wakati nikitekeleza majukumu yangu ya kazi kwenye Kampuni ya
Reli Tanzania, (TRL), na WCF imenilipa fidia ya mkupuo na inaendelea kunilipa pensheni
ya kila mwezi, shilingi 170,000/= kwa maisha yangu yote nitakapokuwa hai.”
Alisema Bw.Fortunatus Kiwale
Naye
Mfanyakazi mwingine wa Kampuni ya Frank Pile International Project Limited ya
jijini Dar es Salaam, Bw. Patrick Millinga, yeye alisema Mfuko umemlipa fidia
ya zaidi ya shilingi milioni 31.9 baada ya kupoteza jicho lake la kushoto
kutokana na kugongwa na kipande cha chuma wakati akitekeleza majukumu yake ya
kazi.
Mwingine
aliyetoa ushuhuda wa faida ya Mfuko kwa wafanyakazi, ni mama mjane, Bi.
Petronila Mligo, ambaye yeye alifiwa na mumewe katika ajali ya gari wakati
akirejea kituo chake cha kazi jijini Mwanza akitokea Dodoma.
“Mfuko
umenilipa fidia ya mkupuo kutokana na kifo cha mume wangu, lakini pia
ninaendelea kulipwa pensheni ya kila mwezi mimi na watoto wangu wawili, ambapo
kila mtoto analipwa shilingi 175,000/= na mimi ninalipwa shilingi 375,000/=.”
Alisema mama huyo mjane ambaye ni mwalimu.
Akiwasilisha
mada mbele ya washiriki, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba alisema
Mfuko unaendeshwa kwa msingi wa utatu ambapo katika bodi ya wadhamini ambayo
ina uwakishi wa serikali, wafanyakazi na uwakilishi wa waajiri kama ambavyo
Shirika la Kazi Duniani linavyotaka katika masuala haya ya fidia kwa
wafanyakazi.
Alisema,
katika mfumo wa zamani, mfanyakazi anapotoka au kwenda kazini endapo atapatwa
na tatizo njiani sheria ya zamani haikumtambua, tofauti na sheria ya sasa ambapo
inaeleza mfanyaakzi akiumia au akifikwa na umauti wakati akitoka kazini au
akielekea kazini sheria ya sasa inataka afidiwe.
“Alisema
Mfuko umeweka utaratibu ili kuhakikisha mfumo wa usajili wa waajiri unakuwa wa
haraka na rahisi lakini pia kushughulikia masuala ya ulipaji fidia katika kipindi
kifupi.” Alisema.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe.
Jenista Mhagama, akihutubia wakati wa mkutano wa wadau wa Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi, (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania,
(TPSF-Tawi la Dodoma) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo
(TCCIA-Tawi la Dodoma), uliofanyika jengo la LAPF mjini Dodoma mwishoni mwa
wiki. Mkuta huo ulioandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, ulilenga kutoa elimu
zaidi kwa wadau na kujadiliana kuhusu namna bora zaidi ya uendeshaji wa shughuli
za Mfuko huo kuhusu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi.
Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu, Bw.Eric Shitindi, akitoa hotuba ya ukaribisho wakati wa mkutano wa
wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania
(ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF-Tawi la Dodoma) na Chama cha
Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA-Tawi la Dodoma), uliofanyika jengo la
LAPF mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Mkuta huo ulioandaliwa na Ofisi ya Waziri
Mkuu, ulilenga kutoa elimu zaidi kwa wadau na kujadiliana kuhusu namna bora zaidi
ya uendeshaji wa shughuli za Mfuko huo kuhsuu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe.
Jenista Mhagama, (Wanne kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi, Bw. Masha Mashomba, (Wakwanza kushoto), wakisalimiana na wanufaika
wa Fidia kwa Wafanyakazi wa (WCF), Bw. Patrick Millinga, (wakwanza kulia) na
Bi. Petronila Mligo, (wapili kushoto), wakati wa mkutano wa wadau wa Mfuko, Chama
cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF-Tawi la
Dodoma) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA-Tawi la
Dodoma, na kufanyika jengo la LAPF mjini Dodoma. Mkuta huo ulilenga kutoa elimu
zaidi na kujadiliana kuhusu namna bora zaidi ya uendeshaji wa shughuli za Mfuko
huo. Wengine pichani ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, (Kazi, Vijana na
Ajira), Mhe. Antony Mavunde, (watatu kulia), Mwakilishi wa ATE, Bw. Almasi
Maige, (wapili kushoto) na Katibu Mtendaji wa TCCIA-Dodoma, Bw.Iddi Senga.
Mkutano ukiendelea
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe.
Jenista Mhagama,(katikati), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi, (WCF), Bw. Mashan Mshomba, (kulia), wakimsikiliza Niabu Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony
Mavunde, wakati wa mkutano wa wadau wa Mfuko, Chama cha Waajiri Tanzania (ATE),
Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF-Tawi la Dodoma) na Chama cha Wafanyabiashara
ya Viwanda na Kilimo (TCCIA-Tawi la Dodoma), uliofanyika jengo la LAPF mjini
Dodoma mwishoni mwa wiki. Mkuta huo ulioandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, ulilenga
kutoa elimu zaidi kwa wadau na kujadiliana kuhusu namna bora zaidi ya
uendeshaji wa shughuli za Mfuko huo kuhusu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi.
Baadhi ya washiriki
Baadhi ya washiriki
Baadhi ya washiriki
Washiriki wakifuatilia hotuba ya Mhe. Waziri.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba akiwa na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalaam Omar, (kushoto) na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bw. Anselim Peter, akijibu baadhi ya hoja zilizojitokeza wakati wa mkutano huo wa majadiliano na wadau.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Eric Shitindi, (kushoto), akiwa na Bw. Mshomba.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, (WCF), Bi. Laura Kunenge, akizungumza jambo wakati wa mkutano huo.
Mhe. Waziri Jenista Mhagama, akizungumza na waandishi wa habari.
Mhe. Waziri akiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wakati akiwasili ukumbini.
Mnufaika wa Fidia, Bi. Petronila Mligo, akitoa ushuhuda wa faida anayopata kutokana na uwepo wa Mfuko, baada ya kufiwa na mumewe akiwa kwenye safarin ya kikazi.
Bw. Patrick Millinga, naye akitoa ushuhuda kutokana na Fidia aliyopata kutoka WCF baada ya kupoteza jicho lake la kushoto wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi.
Mhe. Waziri Mhagama akisalimiana namnufaika mwingine wa Fidia, Bw. Fortunatus Kiwale
Picha ya kwanza ya pamoja.
Picha ya pili ya pamoja.
No comments:
Post a Comment