Na MatukiodaimaBlog WAKATI maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani kwa nchini Tanzania yaliyoandaliwa na shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) yakitaraji kufanyika mkoani Iringa kitaifa mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amesema mkoa wa Iringa kuwa mwenyeji wa mei mosi ni heshima kubwa katika Taifa .
Akizungumza na wanahabari leo ofisini kwake kuhusiana na maandalizi ya Mei Mosi Kitaifa alisema kuwa mkoa wa Iringa umeteuliwa kuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo ambapo mgeni rasmi atakuwa ni Rais Dkt John Magufuli .
Alisema kuwa katika maadhimisho hayo ya Mei Mosi kitaifa kauli mbiu ni Kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii kulenge kuboresha mafao ya wafanyakazi na kuwa kupitia maadhimisho hayo wakazi wa mkoa wa Iringa na wafanyabiashara watapata fursa kubwa ya kujitangaza pamoja na kuonyesha shughuli zao.
Katika maadhimisho hayo ambayo kilele chake kitafanyika uwanja wa Samora mjini Iringa kabla ya kilele kutakuwa na michezo mbali mbali kama mpira wa miguu, kuvuta kamba ,bonanza la michezo tofauti ,mpira wa pete ambayo yote yameanza toka April 17 hadi April 30 mwaka huu .
Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa wa Iringa mwenyeji wa Mei mosi kitaifa mwaka 2018 Bi Amina Masenza alisema sherehe hizo zitahusisha maonyesho ya shughuli ,huduma na bidhaa mbali mbali za wafanyakazi ,taasisi za umma na binafsi ,wawekezaji na wajasiliamali zitakazofanyika uwanja wa Kichangani Kihesa mjini hapa .
Hata hivyo alisema kwa ajili ya kuufanya mkoa wa Iringa uzidi kuwa fursa kwa wageni kutembelea vivutio vya utalii kama hifadhi ya Ruaha na vingine serikali imekaa na wafanyabiashara wa nyumba za kulala wageni na Hoteli ili kuepuka kutumia mei mosi kupandisha gharama za vyumba kwa wagen
Bi Masenza amewataka wananchi wa mkoa wa Iringa na wafanyakazi wote kujitokeza kwa wingi kumlaki Rais wetu mpendwa wetu Dkt John Magufuli .
|
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Juma Masenza |
Rais wa shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Vyamhokya katikati akiongoza kuimba wimbo wa wafanyakazi wakati wa kikao na wanahabari mjini Iringa .
..................................................................................................................................................
No comments:
Post a Comment