Matukio : Naibu Waziri, Dk. Kolimba Akutana na kufanya Mazungumzo na Waziri wa Brazil - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


17 Apr 2018

Matukio : Naibu Waziri, Dk. Kolimba Akutana na kufanya Mazungumzo na Waziri wa Brazil



Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (katikati) akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil, Mhe. Balozi Fernando Jose Marroni de Abreu (hayupo pichani) walipokutana kwa Majadiliano ya Kisiasa yaliyofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Aprili, 2018. Majadiliano hayo yalifanyika wakati wa ziara ya kikazi ya siku mbili ya Mhe. Balozi Fernando hapa nchini. Pamoja na mambo mengine walijadiliana kuhusu namna ya kuboresha mashirikiano ya kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili hususan katika eneo la biashara na uwekezaji.


Pia Naibu Mawaziri hao walijadili namna ya kutekeleza kikamilifu Mradi wa Pamba kwenye eneo la Ziwa Victoria na matokeo ya kusainiwa kwa mkataba wa msamaha wa deni la Tanzania kwa Brazil pia lilijadiliwa. Aidha, Brazil wameahidi kushirikiana na Tanzania kwenye sekta ya afya hususan katika kupambana na maradhi ya Selimundu (Sircle-cell) na kwa upande wa Zanzibar watashirikiana katika afya ya mama na mtoto hususan kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto wachanga.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil, Mhe. Balozi Fernando Jose Marroni de Abreu (katikati) nae akizungumza wakati wa majadiliano ya kisiasa kati yake na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (hayupo pichani). Wengine kwenye picha ni Balozi wa Brazil nchini, Mhe. Carlos Alfonso Iglesias Puente (kushoto) na Mkuu wa Idara inayoshughulikia masuala ya Kaskazini na Mashariki mwa Afrika kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Brazil, Bw. Paulo Cypriano.

Mhe. Dkt. Susan Kolimba akimsikiliza kwa makini Mhe. Fernando de Abreu (hayupo pichani), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil wakati wa Majadiliano ya Kisiasa kati ya Tanzania na Brazil. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Salvator Mbilinyi (kulia)

Mhe. Dkt. Kolimba na Ujumbe wake wakifuatilia mazungumzo hayo
Mhe. Fernando de Abreu na Ujumbe wake wakifuatilia mazungumzo

Mhe. Dtk. Kolimba kwa pamoja na Mhe. Balozi Fernando wakishuhudia uwekwaji saini wa Hati ya Makubaliano kuhusu kuanzishwa kwa Ushirikiano wa Kisiasa kati ya Tanzania na Brazil uliokuwa ukisainiwa na Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi na Balozi wa Brazil nchini, Mhe. Carlos Alfonso Iglesias Puente.

Hati ikisainiwa. Pembeni ya Balozi Nchimbi ni Bw. Mustafa M. Ussi, Afisa Mambo ya Nje kutoka Kitengo cha Sheria .

Mhe. Balozi Nchimbi na Mhe. Balozi Puente wakibadilishana Hati hiyo mara baada ya kusaini huku Naibu Mawaziri wakishuhudia

Mhe. Dkt. Susan akiwa na Mhe. Balozi Fernando mara baada ya kukamilisha majadiliano

Mhe. Dkt. Kolimba (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Fernando (wa nne kushoto). Wengine katika picha ni Balozi wa Tanzania nchini Brazil, mhe. Emmanuel Nchimbi (wa pili kulia), Balozi wa Brazil nchini, Mhe. Carlos Iglesias Puente (wa tatu kushoto), Mkurugenzi wa Kanda ya Ziwa wa Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo ya Kilimo, Dkt. Everina Lukonge (wa pili kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Salvator Mbilinyi (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Jestas Nyamanga

Picha ya pamoja kati ya Naibu Mawaziri na wajumbe wote wa Tanzania na Brazil

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad