Michezo : DC Godwin Gondwe Awafunda Vijana Vibaoni FC ili kutwaa Ubingwa wa Uchumi CUP 2017 -2018 - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


13 Feb 2018

Michezo : DC Godwin Gondwe Awafunda Vijana Vibaoni FC ili kutwaa Ubingwa wa Uchumi CUP 2017 -2018



Mbunge wa Handeni, Omary Kigoda (kushoto) akimkabidhi zawadi ya mipira, Nahodha wa timu ya Kurugenzi Fc, Nguluko Machele, baada ya timu yake kuibuka mshindi wa pili katika michuano ya UCHUMI Cup iliyomalizika jana jumapili katika Uwanja wa CCM Kigoda mji wa Handeni Mkoani Tanga. Michuano hiyo iliandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe (katikati) kwa lengo la kuwahamasisha vijana kujihusisha na Kilimo cha Mihogo na mazao mengine ili kukuza uchumi wa wilaya hiyo. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)


*****************************************
Na Muhidin Sufiani, Handeni
VIJANA wametakiwa kujitambua kukuza vipaji vyao walivyonavyo ili waweze kufika mbali na kuweza kujenga uchumi wa nchi kupitia vipaji.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe, wakati akizungumza katika hafla ya kuhitimisha mashindano ya UCHUMI Cup yaaliyomalizika katika Uwanja wa CCM Kigoda uliopo mji wa Handeni Mkoani Tanga,jana.


Alisema kuwa baada ya mashindano hayo ni mwanzo wa Msimu wa Kilimo na Uelewa wa Vijana kuhusu suala zima la Kilimo cha mihogo ili kuunga mkono kauli ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli ya HAPA KAZI TU na Uchumi wa Viwanda kupitia kilimo.


Aidha alitaka vijana kujitahidi kuwa wawazi katika kutambua na kuweka wazi vipaji vyao ambapo alisema kuwa baada ya kumalizika michuano hiyo na kutambua kuwa mji wa Handeni una vijana wenye vipaji sasa michuano hiyo itakuwa ni endelevu na ili kuhakikisha vijana wanapata nafasi ya kutoka na kucheza soka katika timu kubwa za ligi kuu.


Kwa kuonyesha jitihada hizo Kamati iliyokuwa ikiratibu mashindano hayo kwa kushirikiana na Viongozi wa Chama cha soka Wilayani hapo wamechagua wachezaji nyota kutoka katika kila timu,watakaounda kikosi cha timu ya Wilaya ya Handeni,ambayo itapata fulsa ya kucheza na moja ya timu kubwa ya Ligi kuu ambayo itatangazwa baadaye itakayokuwa tayari kwa ajili ya kuchagua vijana wenye vipaji.


Wakizungumza kwanyakati tofauti wadau mbalimbali wa soka wa Handeni,wamesema kuwa wanamshukuru sana Mhe. Dc Gongwe kwa kuwainua vijana wao katika suala zima la michezo na kusema kuwa michuano kama hiyo sasa imepita miaka 20 na zaidi katika mji huobila kuwa na mashindano ya aina yeyote yanayoleta hamasa kwa vijana.


Aidha wadau hao wamesema kuwa mara ya mwisho mashindano kama hayo yaliwahi kufanywa na aliyewahi kuwa Mbunge wa Handeni Marehemu Dkt.Omary Kigoda, ambapo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza na mwisho kuiona timu ya Simba ikicheza mchezo wa kirafiki katika uwanja huo wa CCM Kigoda.


''Hapa kwa mara ya mwisho kuwa na burudani kama hii ya leo na kushuhudia vijana wetu wakicheza kwa hamasa kubwa katika uwanja huu ilikuwa ni miaka 20 iliyopita ambapo pia tuliwaona Simba enzi hizo kina Julio bado vijana wadogo kabisa wakicheza hapa,lakini tangu hapo hapajawahi kutokea burudan kama hii ya leo,


Kwakweli tunamshukuru sana Mhe. Dc Gondwe kwa ubunifu wake na kuona kuna umuhimu wa kuwainua vijana katika michezo na kujitambua katika Kilimo kwani tuna ardhi nzuri na yenye rutuba ya kutosha wilayani kwetu inayokubari mazao''. alisema mdau wa Soka aliyejitambulisha kwa jina la Esau Ngadala, ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa miguu Wilaya ya Handeni.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Handeni,Asha Kigoda, akimkabidhi zawadi ya Jezi na mipira Kocha wa timu ya Netiboli ya Shule ya Sekondari Kivesa,Shani Salumu,baada ya timu yake kuibuka mshindi wa pili katika michuano ya UCHUMI Cup iliyomalizika jana katika Uwanja wa CCM Kigoda mji wa Handeni Mkoani Tanga. Michuano hiyo iliandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe (katikati) kwa lengo la kuwahamasisha vijana kujihusisha na Kilimo cha Mihogo na mazaomengine ili kukuza uchumi wa wilaya hiyo.

Wachezaji wa timu ya Vibaoni wakishangilia baada ya kukabidhiwa medali zao na Kikombe kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa fainali hizo dhidi ya Kurugenzi.

Mkurugenzi wa handeni, William Kufwe, akimkabidhi zawadi ya mipira na jezi Nahodha wa timu ya Netiboli ya Wanawake Live, Shani Salum, baada ya kuibuka washindi wa kwanza katika mchezo wa fainali za UCHUMI Cup dhidi ya Kivesa Sekondari. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya handeni, Godwin Gondwe.

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa miguu Wilaya ya Handeni, Esau Ngadala, akimkabidhi Tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya UCHUMI Cup, Nahodha wa timu ya Kurugenzi, Nguluko Machele, wakati wahafla ya kukabidhi zawadi kwa timu zilizofanya vizuri katika michuano hiyoiliyomalizika jana katika Uwanja wa CCM Kigoda mji wa Handeni Mkoani Tanga. (katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe.
Nahodha wa timu ya Kurugenzi, Nguluko Machele (katikati) akijaribu kuwatoka mabeki wa Vibaoni, Yusuph Ngole (kulia) na Jumanne Kisuse, wakati wa mchezo wa fainali za michuano ya UCHUMI Cup, iliyomalizika jana kwenye Uwanja wa CCM Kigoda Handeni mkoani Tanga, michuano hiyo iliandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe kwa lengo la kuhamasisha Vijana kujihusisha na Kilimo cha Mihogo na mazao mengine. Katika mchezo huo timu ya Vibaoni ilishinda mabao 3-0 na kutwaa kombe hilo la Uchumi Cup 2017-2018

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad