Maisha : Kazi za Mikono Zawasaidia Wakimbizi Wanawake Kupunguza Makali ya Maisha Kambini - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


11 Jan 2018

Maisha : Kazi za Mikono Zawasaidia Wakimbizi Wanawake Kupunguza Makali ya Maisha Kambini






Baadhi ya wanakikundi Wanawake waishio katika kambi ya Wakimbizi ya Mtendeli iliyopo Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma wakifinyanga vyungu mara baada ya kupata mafunzo kutoka shirika la IRC Ambalo linafadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR) Wanawake hao licha ya kufanikiwa kufinyanga vyungu hivyo, huviuza kwa shilingi 200 kwa kila kimoja, hali ambayo imekuwa haileti tija na faida katika kazi yao.
Mmoja wa wanakikundi wa ufinyanzi katika Kambi ya wakimbizi ya Mtendeli Wilayani Kibondo mkoani Kigoma,ambaye amepata mafunzo kutoka taasisi ya IRC kwa udhamini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi(UNHCR), ambayo yanamuwezesha kutumia muda wake katika shughuli za mikono za uzalishaji.
Ili kuhakikisha uendelevu wa vikundi mbalimbali vya wajasirimali ndani ya Kambi za wakimbizi, kipato hafifu wanachopata baada ya kuuza bidhaa huingizwa katika mfuko wa kuweka na kukopa (VICOBA) wa kikundi ambao umeanzishwa kwa lengo la kuwawezesha wanakikundi kujiwekea akiba pamoja na kugawana faida inayopatikana kila mwisho wa mwezi. Kutokana na wateja kuwa ni watumishi/wadau mbalimbali wanaotembelea kambi hizi faida yao huwa ni finyu.
Mmoja wa Wakimbizi katika Kambi ya Mtendeli Wilayani Kibondo mkoani Kigoma Ambaye amepata mafunzo kutoka taasisi ya IRC kwa udhamini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi(UNHCR). Wanawake hawa wenye uwezo wa kufinyanga vyungu hutumia baadhi ya siku kuwafundisha wanawake wenzao waishio ndani ya kambi hii ya wakimbizi na kwa njia hii elimu inawafikia wanawake wengi. Shughuli za uzalishaji mali/ujasiriamali husaidia kuwajengea wanawake uwezo wa kujikimu kimaisha. Elimu hii itawasaidia hata watakaporejea nchini mwao.

Wanawake wa Kambi ya wakimbizi Mtendeli wakionesha baadhi ya nguo za Watoto ambazo wamezifuma kutokana na uzi kwa kutumia mkono mara baada ya kupata mafunzo kutoka IRC. “Kabla hatujapata haya mafunzo kutokana na mazingira tnayoishi kwa sasa shughuli pekee tuliyoweza kufanya ni kupika na kufanya usafi wa maeneo ya nyumba/mahema lakini sasa tunatumia muda katika kujifunza vitu vya maendeleo.”

Wanawake kutoka Kambi ya Wakimbizi Mtendeli wakifuma Vitambaa kwa uzi kutumia sindano ya mkono mara baada ya kupata mafunzo kutoka Taasisi ya IRC.

Beatrice Emmanuel - Muwezeshaji wa Wanawake kutoka Shirika la IRC linalofadhiliwa na UNHCR, akimvisha mtoto Kofia iliyofumwa na mwanakikundi ndani ya kambi ya Mtendeli

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad