Kushoto aliyevalia koti jeusi ni Mgeni rasmi Mariam Kimoso ambaye alimuakilisha mkurugenzi wa jiji la Arusha akimkabidhi mwalimu aliyefanya vizuri hivi karibuni katika kinyang’anyiro cha kuwasaka walimu bora lililoendeshwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Foundation For Tomorrow jijini Arusha,katikati ni diwani wa kata ya Themi jijini Arusha,Milance Kinabo, (CHADEMA),(Habari Picha na Pamela Mollel-Arusha)
Mkurugenzi wa shirika la Foundation for Tomorrow Melissa Queyquep, akizungumza katika hafla hiyo ambapo alisema kuwa lengo ni kuwawezesha walimu kupata mamlaka ambayo itawasaidia katika ufundishaji wa wanafunzi bila ubaguzi wowote katika kufufua maendelea ya elim
Mgeni rasmi Mariam Kimoso ambaye alimuakilisha mkurugenzi wa jiji la Arusha akizungumza katika hafla hiyo
Walimu wakifatilia hafla hiyo
Mjumbe wa bodi wa shirika la Foundation for Donacian Lyaruu akizungumza katika hafla hiyo
Diwani wa kata ya Themi jijini Arusha,Milance Kinabo, (CHADEMA),akiteta jambo na Bi.Narja Roel
Mwalimu Pius Edward kutoka shule ya msingi Sing’isi akipokea zawadi kwa mgeni rasmi
Mkurugenzi wa Upendo Friends Isabella Mwampamba alisema kuwa mwalimu anatakiwa kuheshimika kwa kazi kubwa ambayo wamekuwa wakifanya hivyo ni muhimu sana kuwatia moyo
Mwenyekiti wa wakuu wa shule jiji la Arusha Msendekwa Reginard akizungumza katika hafla hiyo
Mkurugenzi wa shirika la Foundation for Tomorrow Melissa Queyquep,akimkabidhi zawadi ya T-shirt diwani kata ya Themi jijini Arusha Milance Kinabo
Mkurugenzi wa Upendo Friends Isabella Mwampamba akiteta jambo na Mkurugenzi wa shirika la Foundation for Tomorrow Melissa Queyquep
Picha ya pamoja
Na Pamela Mollel,Arusha
Wadau mbalimbali wa elimu wametakiwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na taasisi ya Foundation for tomorrow katika harakati za kuwapa uwezo walimu pamoja nakuwapa motisha hali ambayo itasaidia wanafunzi kufanya vizuri zaidi wawapo mashuleni
Akizungumza hivi karibu katika Tuzo maalumu ya walimu iliyoandaliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Foundation For Tomorrow, Mgeni rasmi Mariam Kimoso ambaye alimuakilisha mkurugenzi wa jiji la Arusha,alisema kuwa walimu wanakazi kubwa sana hivyo ni vyema wakapongezwa kwa kazi nzuri wanayofanya
Alisema kuwa elimu kubwa inayotolewa na walimu kwa wanafunzi mashuleni itasaidia kuleta mandeleo na jamiii nzima itafaidika kupitia elimu hiyo
Mkurugenzi wa shirika la Foundation for Tomorrow Melissa Queyquep, alisema kuwa lengo ni kuwawezesha walimu kupata mamlaka ambayo itawasaidia katika ufundishaji wa wanafunzi bila ubaguzi wowote katika kufukia maendelea ya elimu
“Mamlaka hayo ni kusimamia mitahala vyema huku walimu ambayo watakaoweza kufanya hivyo kuwapongeza ili wawezekufundisha wanafunzi vyema katika kufikia malengo endelevu kwa wanafunzi”alisema Melissa
Aidha alisema kuwa shirika hilo linalenga katika kuwapa wanafunzi uwezo wa kuchochoea na kuchambua mawazo wawapo mashuleni,kuwasaidia wanafunzi wanaohitahi kujifunza zaidi,
Kwa upande wake mkurugenzi wa Upendo Friends Isabella Mwampamba alisema kuwa mwalimu anatakiwa kuheshimika kwa kazi kubwa ambayo wamekuwa wakifanya hivyo ni muhimu sana kuwatia moyo.
No comments:
Post a Comment