Uchumi : Dk. Ashatu Kijaji Azindua kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Saturday, 16 September 2017

Uchumi : Dk. Ashatu Kijaji Azindua kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango



Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (aliyeshika mkasi) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners handbook), Toleo la Pili, kilichoandikwa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kwa kushirikiana na Taasisi ya Mafunzo ya Jamii ya nchini Uholanzi (ISS), tukio hilo limefanyika katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kampasi ya Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), (katikati), akionesha kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners Handbook), Toleo la Pili, baada ya kukizindua rasmi katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini-Dodoma. Wa pili kushoto ni Kaimu Balozi wa Uholanzi hapa nchini, Bi. Lianne Houben, na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo hicho Prof. Razack Lokina.

Kaimu Balozi wa Uholanzi hapa Nchini, Bi. Lianne Hauben (kushoto), akifurahi wakati akikabidhiwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), nakala ya Kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners Handbook), Toleo la Pili, mara baada ya kukizindua rasmi mkoani Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akimkabidhi Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Razack Lokina, nakala ya Kitabu cha Mwongozo kwa wanamipango (Planners Handbook), Toleo la Pili, mara baada ya kukizindua rasmi mkoani Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akimkabidhi Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya, nakala ya Kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners Handbook), Toleo la Pili, mara baada ya kukizindua rasmi mkoani Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Kanda ya Ziwa, Dkt. Benedict Kilobe, nakala ya Kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners Handbook), Toleo la Pili, mara baada ya kukizindua rasmi mkoani Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akimkabidhi Makamu Mkuu wa Chuo-Mipango, Fedha na Utawala, Dkt. Vedastus Timothy, nakala ya Kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners handbook), Toleo la Pili, kilichozinduliwa katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, mkoani Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akiwaongoza wadau mbalimbali kunyanyua nakala ya kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners handbook), Toleo la Pili, kilichoandikwa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kwa kushirikiana na Taasisi ya Mafunzo ya Jamii ya nchini Uholanzi (ISS), tukio hilo limefanyika katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kampasi ya Dodoma.



Mhadhiri Mstaafu wa Taasisi ya Kimataifa inayotoa elimu ya masuala ya kijamii (The International Institute of Social Studies (ISS), kutoka nchini Uholanzi, Prof. Leo de Haan, akitoa mhadhara kuhusu masuala ya umuhimu wa mipango katika jamii kabla ya kuzinduliwa rasmi kwa Kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners Handbook), Toleo la Pili, tukio lililofanyika katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini-Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati-walioketi), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi wa viongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini pamoja na wahadhiri kutoka Taasisi ya Elimu ya masuala ya Jamii (ISS) ya nchini Uholanzi, baada ya uzinduzi wa Kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners Handbook), Toleo la Pili, tukio lililofanyika katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini-Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)


Benny Mwaipaja, Dodoma
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amezindua Kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango Tanzania, kilichoandaliwa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kwa kushirikiana na Taasisi ya Mafunzo ya Jamii ya nchini Uholanzi (ISS), na kuwataka wataalamu wa mipango hapa nchini kuandaa mipango yenye tija itakayoiwezesha jamii kuondokana na umasikini.


Dkt. Kijaji ameeleza kuwa nafasi ya wataalamu wa mipango katika kukuza uchumi wa nchi ni kubwa na kwamba kinachotakiwa ni kuandaa mipango shirikishi itakayochangia kuimarisha maisha ya wananchi ili waweze kujikwamua kiuchumi.


“Ni matumaini yangu makubwa kwamba kuzinduliwa kwa kitabu hiki cha mwongozo kwa wanamipango, kutakuwa chachu ya wataalamu wetu kuangalia namna ya kupeleka maendeleo vijijini na sehemu nyingine duniani kwa kutoa wataalamu waliobobea ili kuharakisha maendeleo ya nchi” alisistiza Dkt. Kijaji


Ameeleza kuwa maudhui ya kitabu hicho yapelekwe hadi ngazi za chini kupitia Serikali za Mitaa ili watu wengi waweze kukisoma na kuelekezwa namna bora ya kupanga mipango yao ya maendeleo.


Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijini, Prof. Hozen Mayaya, amesema kitabu hicho kimelenga kuwaongezea ujuzi wataalamu wa mipango kwa kuzingatia vitendo zaidi badala ya nadharia.


“Kitabu cha Mwongozo kwa wanamipango kitakuwa rejea ya nadharia nyingi na njia ambazo wataalamu wanapaswa kuzijua, namna ya kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kuifanya mipango iweze kutekelezeka kama ilivyokusudiwa” alisema Prof. Mayaya.


Nae Kaimu Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Bi. Lianne Houben, ambaye kwa namna moja au nyingine nchi yake imefadhili uandishi na uchapaji wa mwongozo huo, toleo la pili, amesema nchi yake inajivunia uhusiano imara uliodumu kwa miongo kadhaa na Tanzania.


Alisema kuwa mtazamo wa ushirikiano wake na Tanzania kuanzia mwaka huu ni kujikita zaidi katika uhusiano wa kibiashara na kiuchumi na kwamba uwekezaji wao mkubwa utalenga pia kuboresha kilimo na usalama wa chakula.


“Uholanzi ni nchi ya pili katika kufanya biashara na Tanzania ikitanguliwa na Marekani ambapo mwaka 2016, Uholanzi, imenunua bidhaa zenye thamani ya Euro bilioni 85” aliongeza Bi. Houben


Aidha, alieleza kuwa nchi yake imetoa mchango mkubwa katika kuendeleza rasilimali watu ambapo hadi sasa wanafunzi na wataalaamu katika fani mbalimbali wapatao 5,000, wamepata mafunzo kutoka katika vyuo mbalimbali nchini Uholanzi.

No comments:

Post a Comment