Afya Zetu : Shilingi Milioni 190 zatumika kutibu ugonjwa wa Kipindupindu ,Iringa - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Wednesday, 20 September 2017

Afya Zetu : Shilingi Milioni 190 zatumika kutibu ugonjwa wa Kipindupindu ,Iringa



Afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya akizungumza na viongozi wa vijiji wa tarafa ya pawaga kuhusu uboreshaji wa vyoo bora kwa lengo la kutatua tatizo la ugonjwa wa kipindupindu ambalo limekuwa likijitokeza mara kwa mara katika tarafa hiyo walianza kutoa elimu kwa viongozi wote na baadae wakahamia kwa wananchi.

Afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya akizungumza na mama moja ambaye hana choo bora na kutundikiwa bendera ilikuwa inamuonyesha kuwa hana choo bora katika kijiji cha mboliboli tarafa ya pawaga mkoani Iringa.
Afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya akisimamia zoezi la utundikaji wa bendera kwa wasio na vyoo bora






Na Fredy Mgunda,Iringa.


Halmashauri ya wilaya ya Iringa imetumia shilingi milioni mia moja na tisini (190,000,000 ) kupambana na tatizo la milipuko ya ugonjwa wa kipindupindu katika tarafa ya pawaga na Idodi mkoani Iringa na ni miongoni mwa halmashauri 156 zinazotekeleza kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira Tanzania bara.


Akizungumza wakati wa utoaji elimu ya matumizi ya vyoo bora katika tarafa ya pawaga afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya aliwataka wananchi kuanza kutumia vyoo bora ili kumaliza tatizo la milipuko ya ugonjwa wa kipindupindu ambao umekuwa ukiwakumba mara kwa mara.


“Jamani chanzo mmoja wapo cha mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ni matumizi ya vyoo ambavyo sio bora hivyo mnatakiwa kutumia vyoo bora na kutoa elimu kwa wananchi wenu maana nyinyi ndi wenye wananchi na leo tunawapa hii elimu nyie viongozi tunaomba muifikishe elimu kwa wananchi”alisema Nkya


Nkya alisema walitoa elimu ya uboreshaji wa miundombinu ya vyoo na kunawa mikono kwa kutumia maji tiririka kwa sabuni mara ya kutoka chooni kwa ngazi ya kaya na shule za msingi na sekondari,Vyuo,taasisi za kidini,taasisi binafsi,taasisi za kiserikali kama ofisi za serikali na vituo vya afya lengo likiwa ni kutokomeza kabisa ugonjwa wa kipindupindu.


“Ukiangalia hadi sana tumefanikiwa kuzifikia jumla ya kaya 24 zilizotekeleza kampeni hiikupitia wadau mbalimbali kama wizara ya afya,wizara ya maji,wizara ya elimu (RWSSP),halmashauri ya wilaya ya Iringa,UNICEFU,SNV na WARID na jumla ya kata nne ambazo ni ilolompya,Mlenge,Mboliboli na Itunundu zimeanza kutekeleza rasmi kampeni hii kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018” alisema Nkya


Mwezi wa pili hadi mwezi wan ne mwaka 2016 ndio kulitokea mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika halmashauri ya wilaya ya Iringa ambapo kata za Mboliboli na Mlenge zilikumbwa na ugonjwa huo huku vijiji vya Luganga,Mnadani,Idodi na Mafuruto vilikuwa na idadi ndogo ya wagonjwa wa kipindupindu.


Aidha Nkya alisema kuwa mikakati ya halmashauri ya wilaya ya Iringa kuzitambua kaya na taasisi zisizo na vyoo bora,kutambua vibarua na wamiliki wa mshamba ya mpunga,kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa usafi wa mazingira vijijini na kutoa elimu ya usafi wa mazingira kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu kisitokee tena katika halmashauri hiyo.


“Tumepeana maagizo ya kutekeleza kama kuwawekea bendera nyekundu kaya na taasisi zote ambazo hazina vyoo bora,kutoa muda maalumu wa kuboresha vyoo vyao vinginevyo kuna faini ambayo itatolewa kwa kaya na taasisi ambazo zitakuwa hazijaboresha vyoo vyao” alisema Nkya


Nyamiki Kimsau ni mwananchi wa kijiji cha Usolanga pawaga alisema kuwa kuwa ugonjwa kipindupindu umekuwa sugu katika kijiji hicho kutokana na wananchi wemgi kutokuwa na vyoo bora ambavyo vinakidhi kuishi na afya bora.


“Wananchi tukiwa tunafanya usafi na kuwa na vyoo bora basi tunaweza kuepukana na milipuko ya ugonjwa wa kipindupindu hivyo naomba serikali kuwa wakali kwenye swala la kuwa na vyoo bora ili kuondokana na aibu ambayo imekuwa inatutafuna kwa muda sasa” alisema Kimsau


Naye Mwaita Bin jumbe alisema kuwa kweli wananchi wa kijiji cha mboliboli hawana vyoo bora kutokana na ugumu wa maisha hivyo wanaomba kupewa muda ili waweze kuboresha vyoo bora lakini swala la ugonjwa wa kipindupindu bado unawakumba kila mara.


“Jamani tunaomba viongozi mtoe elimu ya kutosha kwa wananchi ili wajue umuhimu wa kuwa na vyoo bora tofauti na hali iliyopo hivi sasa” alisema Bin jumbe


Hamis Matyame ni kijana wa kijiji cha mboliboli aliita serikali ya kijiji kutafuta njia mbadala ya kuwachimbia vyoo bora wazee ambao hawana uwezo wa kifedha na guvu kazi kwa sababu wasipo saidiwa ugonjwa wa kipindupindu hauta koma katika tarafa ya pawaga.


“Mimi kama kijana napenda kuwasaidia wazee kuboresha vyoo ila hapa kijijini kuna wazee wengi hivyo pekee yangu siwezi hivyo naiomba serikali kutafuta njia mbadala kuwasaidia hawa wazee” alisema Matyame

No comments:

Post a Comment