Matukio : Wakati Umefika Wanawake Kuajiri na Kufukuza - Mongela - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Saturday, 12 August 2017

Matukio : Wakati Umefika Wanawake Kuajiri na Kufukuza - Mongela


Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika, Getrude Mongela amesema wakati umefika kwa wanawake kuajiri na kufukuza. Alitoa kauli hiyo katika sherehe za Uzinduzi wa Jukwaa la Kuwaendeleza Wanawake Afrika (WAA) iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Jukwaa hilo linasimamiwa na Taasisi ya Graca Machel. Mama Mongela alikuwa akijibu maswali ya waandishi kuhusiana na hisia zake baada ya uzinduzi na majadiliano ya Kitabu “Women Creating Wealth” ambazo ni simulizi la wanawake wajasiriamali katika bara la Afrika, waliofanikiwa na safari yao katika ujasiriamali. Alisema ingawa wakati wa Mwalimu Nyerere juhudi zilifanyika kuwawezesha wanawake, kundi hilo lilibaki kufanyakazi za kufungasha au kushona, lakini kizazi cha sasa kimeendelea kiasi ya kwamba kina uwezo wa kufanya uwekezaji na kuwa waajiri. Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika, Getrude Mongela akifanya mahojiano na mwandishi wa kituo cha Televisheni cha ITV, Henry Mabumo mara baada ya uzinduzi wa kitabu cha Kitabu “Women Creating Wealth” wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Jukwaa la Kuwaendeleza Wanawake Afrika (WAA) iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Jukwaa hilo linasimamiwa na Taasisi ya Graca Machel.(Picha zote na Thebeauty.co.tz) Alisema amefurahishwa sana na maelezo ya ndani ya kitabu hasa safari mbalimbali za wanawake kuanzia vijana na wale wa kati ambao wamethubutu na kuonesha njia ya ujasiriamali bila kukata tamaa na hivyo kuwa mfano kwa wengine. Alisema katika mahojiano hayo kuwa wanawake kwa sasa wakati umefika wa kuwa na viwanda vikubwa, kumiliki na kuwezesha mabadiliko ambayo yatachochea maendeleo binafsi, familia na hata taifa. Anasema wanawake waliachwa nyuma kutokana na wanaume kutotambua au kutokubali uwezo wa mwanamke na sasa vijana wanaonesha kwamba wanawake wanaweza na wanathubutu. Mshereheshaji wa uzinduzi wa kitabu cha Kitabu “Women Creating Wealth” Mwasisi wa Re-Write, Chidiogo Akunyili akisherehesha uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.[/caption] Pamoja na kazi hizo amesema wakati umefika wa wanawake kutumia akili ili siku moja kipuri kitengenezwe na mdada na watu wajisikie fahari kwenda kukitumia. Akizungumzia kitabu hicho Mwasisi wa mtandao wa She Inspires Her, Lisa O'Donoghue-Lindy amesema kwamba kinatoa maelezo ya safari ya wajasiriamali wa kike, dhiki zao, changamoto na namna walivyoanzisha ujasiriamali wakati mwingine wakiwa na fedha kidogo kiasi cha dola 23 katika mifuko yao. Alisema kitabu hicho kimeandaliwa kutoka wajasiriamali mbalimbali takribani 60 wa bara la Afrika kwa lengo la kutoa hamasa kwa wajasiriamali wengine ambao wanachipukia au wale ambao wanataka kuthubutu. Muasisi wa mtandao wa She Inspires Her, Lisa O'Donoghue-Lindy akielezea yaliyomo kwenye kitabu cha "Women Creating Wealth” ambacho ni simulizi za wanawake 60 wajasiriamali katika bara la Afrika, waliofanikiwa na safari yao katika ujasiriamali. Alisema kwamba maelezo yaliyomo ndani ya kitabu hicho ni binafsi mno, kwani walizungumzia ubunifu na safari ya kiuchumi waliyoianzisha wadada hao na namna waliyvoondoka katika changamoto mbalimbali. Aidha kimelenga kushawishi watoa maamuzi kutoa nafasi ya wanawake kuendelea na kuona umuhimu wao katika kuimarisha maendeleo na usawa. Miongoni mwa watu waliomo ndani ya kitabu hicho Jacqueline Mengi, Esther Karin Mngodo, Devotha Minzi na Mtendaji wa kampuni ya uhandisi ya Mount Carmel Seline Mwenelupembe. Wapo pia wajasiriamali kutoka Kenya, Uganda na Kongo ya Kinshasa. Akizungumza kuhusu kuwamo katika kitabu hicho Jacqueline Mengi alisema anajisikia furaha kuwa mfano wa kuwafundisha wengine, akisema kwamba anaona fahari kuwaambia wanawake wenzake kwamba kujiamini ni silaha muhimu na kwamba ukishinda nafsi ni lazima ufanikiwe. Mtendaji wa kampuni ya uhandisi ya Mount Carmel Ltd Seline Mwenelupembe ambaye ni mmoja wa wanawake wajasiriamali waliomo ndani ya kitabu hicho akielezea safari yake ya ujasiriamali ambapo mpaka sasa ametoa ajira ya kudumu kwa watu 50 nchini kwake.Aliwataka wanawake kushikamana na kupeana ushirikiano katika safari hiyo. Naye Renee Ngamau Mtangazaji wa redio kipindi cha Capital in the Morning kutoka kampuni ya Capital Group Limited alitoa hongera kwa kukazabuti kwa washiriki wote waliomo katika kitabu kwamba wamefanyakazi moja muhimu ya kuonesha wanawake kwamba ujasiri na uthubutu ni kitu cha muhimu katika kuamua maisha yao binafsi. Alisema wanawake hao wameonesha kwamba kwa hali yoyote ile mwanamke akifanya maamuzi ya kuendelea mbele ataweza. Anasema wanawake ndio msingi mkubwa wa maendeleo kwa kuwa asilimia 90 ya pato lao hulirejesha katika familia kwa shughuli mbalimbali za kijamii. Mtangazaji wa redio kipindi cha Capital in the Morning kutoka kampuni ya Capital Group Limited, Renee Ngamau akitoa pongezi kwa washiriki waliomo katika kitabu cha “Women Creating Wealth” wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho. Akielezea siri ya mafanikio yake Devotha Minzi ambaye kwa sasa ana kampuni ya ushauri kuhusu namna ya kuingia katika ujasiriamali, alisema kwamba mambo ambayo yamekuwa yakimfikirisha sana ni kuhusu namna ya wahitaji wanavyoweza kupata fedha benki na wala si benki kutoa fedha. Minzi ambaye aliwahi kuajiriwa Benki Kuu aliacha kazi yake hiyo na kuingia katika kuwekeza katika taasisi ya fedha kabla ya kuachana nayo na kuanzisha kampuni ya ushauri. Akizungumza katika mkutano huo alisema kwamba wakati anaingia katika ujasiriamali alitambua kwamba kuna shida ya kujiweka sawa kuchukua fedha za Benki na hivyo kuona haja ya kuwapa elimu wanawake kuhusu Benki kuwapa fedha na si kunung’unika kwamba hawapewi fedha. Mwanauchumi Devotha Minzi akielezea siri ya mafanikio yake wakati wa uzinduzi wa kitabu cha “Women Creating Wealth” kilichoandaliwa na Taasisi ya Graca Machel uliofanyika jijini Dar es Salaam.Alisema ni vyema wanawake kufanyakazi zao kwa akili zaidi na kuhakikisha kwamba wamejiandaa vyema katika kuhakikisha kwamba mahitaji yao yanatekelezeka kwa kutambua mambo ambayo ni muhimu katika uwekezaji na kuwa na nguvu. Anasema mpaka alipofika yeye amekumbana ana changamoto nyingi lakini la maana ni kuwa ana ratibu na anaangalia zaidi mahitaji na taratibu zake akiongeza kwamba kwa sasa amejikita kutoa ushauri wa kuwawezesha wanawake wenzake kukopesheka. Mkurugenzi wa Amorette Ltd, Jacqueline Mengi na Mtaalamu wa masuala ya fedha na CEO wa Philips Tanzania, Monica Joseph wakifurahi jambo wakati wa uzinduzi huo.[/caption] Alisema ni vyema watu wakabadilika kifikra na kutengeneza utaratibu ambao utawafanya benki wawape hela bila hata kuombwa. Katika jukwaa hilo wanawake walipata nafasi pia ya kuhutubiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambaye aliwataka wanawake kusaidia serikali katika kuhakikisha uchumi unakua. Mkurugenzi wa Amorette Ltd, Jacqueline Mengi na baadhi wanawake wenzake wajasiriamali wakitambulishwa kwenye uzinduzi huo. Mkurugenzi wa Amorette Ltd. Mama Jacqueline Mengi na CEO wa Philips Tanzania, Monica Joseph katika uzinduzi huo. Baadhi ya wanawake wajasiriamali kati ya 60 kutoka bara la Afrika ambao simulizi zaoza safari ya ujasiriamali zimo katika kitabu cha “Women Creating Wealth” kilichoandaliwa na Taasisi ya Graca Machel wakiwa kwenye picha ya pamoja akiwemo Mama Jacqueline Mengi. Muasisi wa Taasisi ya Graca Machel, Graca Machel katika picha ya pamoja na wanawake wajasiriamali kati ya 60 waliondikwa kwenye kitabu cha “Women Creating Wealth” kilichoandaliwa na Taasisi ya Graca Machel. Muasisi wa Taasisi ya Graca Machel, Graca Machel akiwapongeza wakinama hao mara baada ya picha ya pamoja. Mkurugenzi wa Amorette Ltd, Jacqueline Mengi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa kitabu hicho. Muonekano wa nje wa Kitabu cha “Women Creating Wealth” ambacho kinasimulizi za wanawake wajasiriamali katika bara la Afrika, waliofanikiwa na safari yao katika ujasiriamali akiwemo Mama Jacqueline Mengi. Ukurasa wa ndani ya kitabu cha “Women Creating Wealth” ambao umechapisha simulizi za safari ya ujasiriamali ya Mkurugenzi wa Amorette Ltd, Jacqueline Mengi.[/caption] Muasisi wa Taasisi ya Graca Machel, Graca Machel akisalimiana na kumpongeza Mkurugenzi wa Amorette Ltd, Jacqueline Mengi mara baada ya uzinduzi wa kitabu cha “Women Creating Wealth” uliofanyika jijini Dar es Salaam. Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika, Getrude Mongela (aliyeipa mgongo kamera) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Amorette Ltd, Jacqueline Mengi (wa tatu kushoto) Mkurugenzi wa Shule Direct, Faraja Nyarandu (wa pili kushoto), Mmiliki wa duka la ENJIPAI, Nasreen Kareem (kushoto) wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu cha “Women Creating Wealth” uliofanyika jijini Dar es Salaam. "Ha ha ha Wanawake tunaweza" Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika, Getrude Mongela wakipongezana kwa furaha isiyo kifani na Mkurugenzi wa Amorette Ltd. Mama Jacqueline Mengi wakati wa uzinduzi huo. Mkurugenzi Mtendaji wa IBRA Construction Limited Bi. Maida Waziri Juma ambaye pia ni miongoni mwa wanawake 60 walitoa simulizi za kufanikiwa na safari yao katika ujasiriamali. Muasisi wa Taasisi ya Graca Machel, Graca Machel katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shule Direct, Faraja Nyalandu mara baada ya uzinduzi wa kitabu hicho.

No comments:

Post a Comment