Matukio : Prof. Elisante Awataka Maafisa Utamaduni kutangaza Vivutio vya Kiutamaduni Vilivyopo katika Mikoa yao - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Wednesday, 23 August 2017

Matukio : Prof. Elisante Awataka Maafisa Utamaduni kutangaza Vivutio vya Kiutamaduni Vilivyopo katika Mikoa yao






Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiongea na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro jana wakati wa ziara yake ya kikazi ambapo aliwataka watumishi wawe na utamaduni wa kufanya kazi kwa kushirikiana na wananchi.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo akieleza umuhimu wa filam katika kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja na taifa kwa ukumla wakati wa kikao na Maafisa Utamaduni na watendaji wa Mkoa wa Morogoro.


Wajumbe wa kikao wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (Hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi jana mkoani Morogoro.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiongea na baadhi ya Wazee wa kimila wa Mkoa wa Morogoro wakati wa ziara yake ya kikazi jana Mkoani hapo.

Baadhi ya wazee wa kimila wa Mkoani Morogoro wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (Hayupo pichani) alipofanya ziara ya kikazi jana mkoani hapo.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (Kulia) akimsikiliza Makamu Mkuu wa Chuo cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Utawala na Fedha Dkt. Yonika Ngaga (kushoto) alipotembelea makaburi ya Wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini yaliyopo Mazimbu Morogoro wakati wa ziara yake ya kazi jana mkoani hapo.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa fundi bombo Idara ya Matengenezo Chuo cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Bw. Ally Mkopi alipotembelea makaburi ya Wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini yaliyopo Mazimbu mkoani Morogoro wakati wa ziara yake ya kazi jana mkoani hapo.
(Picha na Lorietha Laurence –WHUSM).

No comments:

Post a Comment