Afya : MUWSA Yawasogezea huduma ya Maji kijiji cha Newland Wilayani Moshi - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Wednesday, 9 August 2017

Afya : MUWSA Yawasogezea huduma ya Maji kijiji cha Newland Wilayani Moshi



Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Prof Kitila Mkumbo akitia saini katika kitabu cha wageni alipotembelea Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) kwa ajili ya uzinduzi wa mradi wa Maji katika kijiji cha Newland.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Joyce Msiru akizungumza wakati wa utamburisho wa wajumbe wa Bodi ya Mamlaka hiyo kwa katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Prof Kitila Mkumbo alipotembelea Mamlaka hiyo.

Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa MAzingira mjini Moshi (MUWSA) .

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof,Kitila Mkumbo katika eneo la Shabaha kwa ajili ya uzinduzi wa tanki la Maji linalohifadhi maji kwa ajili ya wakazi wa kijiji cha Newland.

Tenki la kuhifadhia Maji kwa ajili ya Mradi wa Maji yanayosambazwa katika kijiji cha Newland.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Utalii,Prof Kitila Mkumbo akizindua tenki la Maji katika eneo la Shabaha kwa ajili ya wakazi wa kijiji cha Newland.kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakuruenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Prof Faustine Bee na kushoto mwa katbu Mkuu ni Mjumbe wa Bodi hiyo ,Bi Hajira Mmambe.






Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji ,Prof Kitila Mkumbo akiwabebesha maji wawakilishi wa wananchi wa kijiji cha Newland mara baada ya kuzindua mradi wa maji katika eneo hilo.

Diwani wa kata ya Mabogini kilipo kijiji cha Newland ,Emanuel Mzava akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji hicho ambacho wakazi wake wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji katika kijiji hicho.




Baadhi ya Viongozi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) wakiwa katika uzinduzi huo.

Baadhi ya wafanyakazi wa MUWSA wakiwa katika uzinduzi huo.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi ,(MUWSA) Joyce Msiru akitoa taarifa ya Mamlaka hiyo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji ,Prof ,Kitila Mkumbo (Hayupo pichani) alipofanya uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Newland.

Mkurugenzi MUWSA ,Joyce Msiru akikabidhi taarifa kwa katibu Mkuu Wizara ya maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Prof ,Faustine Bee akizungumza kaika uzinduzi huo.

Mjumbe wa Bodi a Wakurugenzi wa MAMLAKA YA mAJI SAFI NA uSAFI WA mazngira mjini Moshi(MUWSA) Hajira Mmambe akisalimia wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wa katika kijiji cha Newland.


Katibu tawala mkoa a Kilimanjaro na Mjumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Mhandisi ,Aisha Amour akitoa salamu wakati wa uzinduzi wa mradi huo.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Prof Kitila Mkumbo akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji safi katika kijiji cha Newland kilichopo kata ya Mabogini wilaya ya Moshi.


Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Newland akicheza kwa furaha baada ya maji kuanza kutoka katika kijiji hicho.



Kikundi cha Burudani cha Msanja kikitoa burudani wakati wa uzinduzi wa mradi wa majisafi katika kijiji cha Newland kilichopo kata ya Mabogini wilaya ya Moshi.


Na Dixon Busagaga wa Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment