Matukio : Yeyote Atakayekamatwa na Bima Feki Sheria Itachukua Mkondo wake - TIRA - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


14 Jul 2017

Matukio : Yeyote Atakayekamatwa na Bima Feki Sheria Itachukua Mkondo wake - TIRA



Mwanasheria Arthur Mbena kutoka Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) akiwa katika maonyesho ya 41 ya biashara Kimataifa sabasaba. sabasaba jijini Dar es salaam.

Bango la Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini lenye maelezo namna ya kutambua bima kama ni halali au ni feki kama maelezo yanavyosomeka hapo .

Wa kwanza kushoto ni Mwanasheria Arthur Mbena akiwana Paul Abdiel ambae ni Afisa Mchambuzi (Bima)kutoka (TIRA)Makao makuu Dar es salaam wakiwa katika maonyesho ya 41 ya biashara Kimataifa sabasaba.

Wa kwanza kushoto ni Mwanasheria Arthur Mbena akiwana Paul Abdiel ambae ni Afisa Mchambuzi (Bima)kutoka (TIRA)Makao makuu Dar es salaam wakiwa katika maonyesho yakatika maonyesho ya 41 ya biashara Kimataifa sabasaba. wakiwa wanatoa elimu kwa mteja aliyetembelea banda hilo katika maonyesho haya.



Na,Vero Ignatus Dar es salaam.


Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini( TIRA)imetoa rai kwa wananchi kutumia mfumo wa TIRA MIS ambao utamsaidia mteja kutambua bima za vyombo vya moto zenye uhalali au feki kwa kutumia mfumo wa kieletroniki.




Hayo yamesemwa na mwanasheria Arthur Mbena ambapo amesema kuwa mtu yeyote yule ambae atakamatwa na bima feki sheria itafuata mkondo wake, ameainisha njia ambazo mtu anaweza kutambua bima yake kama ni feki ama halali kwa kutumia simu ya mkononi( smart phone)kutumia mtandao http/mis.tira.go.tz,google unadownlod tira mis.




Aidha amesema kuwa kazi kubwa ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini ni kuwa msimamizi wa sekta ya Bima mwenye kiwango kinachokubalika Kimataifa,kuendeleza ,kukuza masoko ya Bima imara,shirikishi lenye kuthamini usawa na utendaji mahiri,kwa manufaa na kulinda maslahi ya wateja.




Kwa upande wake Afisa Mchambuzi (Bima)kutoka (TIRA) Paul Abdiel amesema kuwa mamlaka hiyo inafanya shughuli zake kwa weledi, kuwapa kipaumbele wateja ,ushirikiano ,kuwajibika ,pamoja na kuaminika na uwazi




Amewataka wateja wa Bima za vyombo vya moto kuwa makini pale wanapokatiwa Bima hizo wazihakiki na kuhakikisha kama ni halali ama la.

Wananchi wakiwa wanaingia katika banda la Wizara ya Maliasili na utralii kama inavyoonekana pichani .




Baadhi ya wananchi kama inavyoonekana pichani wakiwa katika maonyesho hayo ya 41 ya Biashara ya Kimataifa sabasaba .Picha na Vero Ignatus blog

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad