Matukio : Mwakilishi wa Jimbo la Tungu Ashiriki Ujenzi wa Soko la Samaki - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 24 July 2017

demo-image

Matukio : Mwakilishi wa Jimbo la Tungu Ashiriki Ujenzi wa Soko la Samaki


DSC_0740
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akiwa na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Khalafa Salum Suleima wakishiriki katika ujenzi wa Taifa wa kujenga Soko la Samaki katika ufukwe wa pwani ya Kijiji cha Tindini Unguja Ukuu Zanzibar Wilaya ya Kati Unguja, wakikata majengo ya kuezekea bati katika soko hilo. Pia wamekabidhi mabati kwa ajili ya ujenzi huo ili kutowa mazingira mazuri ya Soko hilo wakati wa kufanya mnada wa samaki kwa wavuvi wanaporudi baharini kuvua.
DSC_0751
Wananchi wa Kijiji cha Tindini Unguja Ukuu wakishirikiana na Mbunge wao na Mwakilishi katika ujenzi wa Taifa wa Soko la Samaki katika ufukwe wa Bahari ya Unguja Ukuu Zanzibar.DSC_0707
Mbunge nas Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said ma Mhe Khalifa Salum Suleiman wakikabidhi mabati kwa Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Bi. Sauda Ramadhani, hafla hiyo ya makabidhiano ya Mabati hayo na miti yamefanyika katika viwanja vya Soko hilo Kijiji cha Tindini Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja Mkoa wa Kusini.
DSC_0471
Wananchi wa Kijiji cha Tindini wakishiriki katika ujenzi wa Soko la Samaki Tindini likiwa katika hatua ya kuezeka.na kuhudumiwa wananchi wavuvi wa kijiji hicho kuuzia samaki wao..
DSC_0474 Wananchi wa Kijiji cha Tindini wakishiriki katika ujenzi wa Soko la Samaki Tindini likiwa katika hatua ya kuezeka.na kuhudumiwa wananchi wavuvi wa kijiji hicho kuuzia samaki wao

DSC_0490
Kiongozi wa Kijiji cha Tindini akitowa maelezo ya ujenzi wa Soko hilo la Samaki katika ufukwe wa bahari yao litakalotowa huduma ya kuuzia samaki kwa wavuvi katika soko la mnada.
DSC_0515
Mwakilishi wa Jimbo las Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Soko la Samaki katika kijiji cha Tindini Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja na kuwataka wananchi wa maeneo hayo kulitumia soko hilo kwa shughuli zao za biashara ya samaki na minada kwa wavuvi wanaorudi bahari kuvua.
DSC_0535
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar akisisitiza jambo wakati wa hafla hiyo kwa Wananchi wa Jimbo lake.
DSC_0548
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja Bi Sauda Ramadhani akizungumza wakati wa hafla hiyo ujenzi wa taifa na kukabidhi mabati na vifaa vya ujenzi wa Soko la Samaki katika Kijiji cha Tindini Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja. DSC_0492

Wananchi na wavuvi wa kijiji cha Tindini Unguja Ukuu wakimsikiliza mgeni rasmin wakati wa hafla hiyo ya ujenzi wa Taifa na kukabidhi mabati kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Soko hilo.
DSC_0714
Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge na Mwakilishi na Wananchi wa Kijiji cha Tindini Unguja Ukuu baada yas hafla hiyo.
Imetayarishwa na Othman Mapara.Blogspots.com
Zanzinewes.com.
Email.othmanmaulid@gmail.com

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *