Matukio : Mazishi ya Linah Mwakyembe kufanyika leo Kijijini Ikolo, Wilayani Kyela Mkoani Mbeya - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


19 Jul 2017

Matukio : Mazishi ya Linah Mwakyembe kufanyika leo Kijijini Ikolo, Wilayani Kyela Mkoani Mbeya


Jeneza lenye mwili wa Marehemu Linah George Mwakyembe aliyekuwa Mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, ukiwa nyumbani kwao katika Kijiji cha Ikolo, wilayani Kyela mkoani Mbeya. mwili wa Marehemu Linah George Mwakyembe unatarajiwa kuhifadhiwa kwenye nyumba yake ya Milele mchana huu katika Makaburi ya familia, Kijijini kwao Ikolo, wilayani humo.

Prof. Mark Mwandosya na Mkewe Bi. Lucy Mwandosya wakiwafariji watoto wa Marehemu wakati waliopofika msibani hapo mapema leo.

Prof. Mark Mwandosya akimfariji Dkt. Harrison Mwakyembe aliyefiwa na Mkewe, Linah George Mwakyembe wakati maandalizi ya mazishi yake, Kijijini kwao Ikolo, wilayani Kyela mkoani Mbeya. Kushoto ni Mke wa Prof. Mwandosya, Bi. Lucy Mwandosya.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akilakiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel alipowasili nyumbani kwa Dkt. Harrison Mwakyembe, Kijijini Ikolo, wilayani Kyela, tayari kwa Mazishi ya Marehemu Linah George Mwakyembe aliyekuwa Mke wa Dkt. Mwakyembe.

Wakuu wa Mikoa ya Lindi na Njombe, Godfrey Zambi (kushoto) na Ole Sendeka (kulia) wakiwasili nyumbani kwa Dkt. Harrison Mwakyembe, Kijijini Ikolo, wilayani Kyela.Post Top Ad