Matukio : Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan Amrithi Mama Salma Kikwete Ulezi wa Tanzania Girl Guides - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Wednesday, 12 July 2017

demo-image

Matukio : Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan Amrithi Mama Salma Kikwete Ulezi wa Tanzania Girl Guides


Na Abraham Ntambara.
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wasichana ambo ni wanachama wa chama cha Tanzania Girl Guides Association (TGGA) kuzingatia mafunzo wanayopatiwa kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.
Kauli hiyo aliitoa leo jijini Dar es Salaam wakati akikabidhiwa kijiti cha kuwa mlezi wa chama hicho kutoka kwa Mama Salma Kikwete anayesitaafu nafasi hiyo aliyoihudumu kwa zaidi ya miaka 12.
“Niwatake tu watoto wangu kutochukulia kwa mzaha mafunzo mnayopatiwa kwani ni tija kwa maendeleo ya Taifa,” alisema Makamu wa Rais.
Aidha aliwaahidi wanachama kutowaangusha katika kutekeleza majukumu ya kukilea chama hicho ambapo alimpongeza Mama Salma Kikwete kwa kuweza kukiongoza vizuri kwa mafanikio makubwa licha ya kuwa na majukumu mengine.
Aliahidi kuifanyia kazi changamoto iliyotajwa ya matumizi ya mitandao ya kijamii ambapo alisema atalisimamia hilo kwani ni vizuri kutumia mitandao hiyo kwa kuzingatia maadili kutokana na hivi sasa watu kuitumia vibaya.
Pia alitoa pendekezo la chama hicho kubuni miradi mingine ambayo inaweza kuwaingizia fedha ili kuacha kutegemea wahisani. Mama Salma Kikwete wakati akimuachia jukumu hilo la kukilea chama hicho alimkabidhi vitu vitatu ambavyo ni Bendera ya Taifa ya chama, Katiba na mpango mkakati wa chama na kumvalisha Skafu ya chama kama ishara ya kukabidhiwa rasmi kijiti hicho.
Aidha alisema kuwa chama kimekuwa na mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuweza kuongeza wanachama kutoka 97,143 hadi kufikia wanachama 100,008 mwaka huu.
Aliongeza kwamba wanatarajia mwezi Septemba kuapisha wanachama 300 katika mkoa huku akieleza kwamba tayari wamekwisha sajili zaidi ya wanachama 2000 katika mkoa wa lindi.


IMG_9724
Aliyekuwa Mlezi wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Mama Salma Kikwete (kushoto) akimkabidhi Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan bendera ikiwa ni ishara ya kumpatia ulezi wa chama hicho katika hafla iliyofanyika, kwenye viwanja vya Jumba la Makumbusho Dar es Salaam leo
.


01
Mama salma akimkabidhi Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mpango mkakati wa TGGA
02
Samia Suluhu Hasan akimkabidhi Mlezi mstaafu wa TGGA zawadi ya saa aliyopewa zawadi na uongozi wa TGGA kwa ajili ya kumbukumbu. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA - KAMANDA WA MATUKIO BLOG
IMG_9533
Kikundi cha sanaa cha Ilala kikitumbuiza
IMG_9545
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, ambaye pia ni Kamishna wa TGGA, Sophia Mjema akimlaki aliyekuwa Mlezi wa TGGA Mama Salma Kikwete
IMG_9553
Mama Salma Kikwete akisalimiana na Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi
IMG_9554
Salma Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba
IMG_9571
Mama Salma Kikwete akisalimiana na Kamishna wa TGGA



IMG_9596
Samia akiangalia kazi mbalimbali zinazofanywa na Girl Guides
IMG_9602


IMG_9604
Samia akipata maelezo kutoka kwa Mkufunzi wa Girl Guides Ruth kuhusu kazi mbalimbali za TGGA
IMG_9620
Samia na Salma Kikwete wakilakiwa na Girl Guides
IMG_9639
Brass Band ya Polisi ikiongoza wimbo wa Taifa
IMG_9650
Viongozi mbalimbali wakiwa katika sherehe hiyo
IMG_9652
Baadhi ya makamishna wa TGGA wakiwa katika sherehe hiyo
IMG_9657
Mwenyekiti wa TGGA Profesa Martha Qorro akitambulisha baadhi ya wageni waalikwa
IMG_9664
Kamishna Mkuu wa TGGA Symphorosa Hangi akisema neno la utangulizi pamoja na kutambulisha wageni waalikwa
IMG_9685
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TGGA, Anna Abdalah akihutubia wakati wa sherehe hiyo
IMG_9693
Aliyekuwa Mlezi wa TGGA, Mama Salma Kikwete akihutubia kabla ya kumkabidhi ulezi Makamu wa Rais Samia
IMG_9702
Ni furaha iliyoje
IMG_9743
Salma Kikwete akimvisha skavu Mlezi mpya wa TGGA, Samia Suluhu Hassan

IMG_9778
Wasanii wa Shule ya Msingi Umoja wakitumbuiza wakati wa sherehe hiyo


IMG_9848
Ni wakati wa furaha


IMG_9791
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mjema na Mwenyekiti wa Bodi ya TGGA, Anna Abdalah wakichenza ngoma

IMG_9793

IMG_9797
Mama Samia akimtunza fedha kiongozi wa kikundi cha Umoja kwa kucheza vizuri
IMG_9808
Kamishna Mkuu wa TGGA akimkabidhi zawadi ya saa Mlezi mstaafu wa TGGA, Mama Salma Kikwete
IMG_9832
Mama Salma akionesha Saa hiyo
IMG_9858


IMG_9861
Girl Guides wakighani shairi maalumu
IMG_9887
Baadhi ya makamishna wakiimba wimbo maalumu
IMG_9890
NI FURAHA TELE
IMG_9893
Viongozi na makamishna wakiwa katika picha ya pamoja na Mlezi mpya wa TGGA, Samia
IMG_9895
Mlezi mpya, Mama Samia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na makamishna wa mikoa
IMG_9898
Mama Samia na Salma Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TGGA
IMG_9900
Girl Guides wakiwa na Mama Salma Kikwete pamoja na Mlezi mpya, Samia
IMG_9902

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *