Matukio : Taswira mbalimbali za Kuagwa kwa Mwili wa Mzee Philemon Ndesamburo, Moshi Kilimanjaro - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


7 Jun 2017

Matukio : Taswira mbalimbali za Kuagwa kwa Mwili wa Mzee Philemon Ndesamburo, Moshi Kilimanjaro




Gari lililobeba mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo likielekea kwenye kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kiboriloni kwa ajili ya kuombewa. Maziko ya Marehemu Ndesamburo yanafanyika leo nyumbani kwake mtaa wa KDC- Moshi,mkoani Kilimanjaro.

Gari lililobeba mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo likiingia kwenye kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kiboroloni.

Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe akiiingia katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kiboroloni kwa ajili ya kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo.


Viongozi mbali mbali wa Chadema wakiingia katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kiboriloni.

Viongozi mbali mbali wa Chadema wakiingia katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kiboriloni. Waziri mkuu wa Zamani ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa akiingia kanisani.

Wabunge wa Chadema wakiwa wamejipanga kupokea mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kiboriloni.

Wajukuu wa Marehemu Phillemon Ndesamburo wakielekea kanisani.


Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo ukiingizwa kanisani.

Waziri mkuu wa Zamani ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa akibadilishana mawazo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi katika ibada ya kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo.

Viongozo wa Chadema wakiwa katika ibada ya kumuombea aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo.

Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo ukiwa kanisani tayari kwa maombezi.

Mke wa Marehemu aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo (wa pili toka kushoto) akiwa kanisani.




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad