Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Balozi Abdulcisco Omar Mtiro almarufu kama CISCO likiwa nyumbani kwake Mikocheki B, Jijini Dar es salaam tayari kwa ibada ya kuuaga mwili kabla ya kwenda kuuhifadhi kwenye Nyumba yake ya Milele, katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar mchana huu.
Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir akizungumza machache kabla ya kuuswalia Mwili wa Marehemu Balozi Abdulcisco Omar Mtiro almarufu kama CISCO nyumbani kwake Mikocheki B, Jijini Dar es salaam.
Rais Mstaafu, Alhaj Ally Hassan Mwinyi akijumuika na viongizi wastaafu wa Serikali katika Msiba wa Marehemu Balozi Abdulcisco Omar Mtiro almarufu kama CISCO nyumbani kwake Mikocheki B, Jijini Dar es salaam.
Kisomo cha kumuombea Marehemu Balozi Abdulcisco Omar Mtiro almarufu kama CISCO kikiendelea nyumbani kwake Mikocheki B, Jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment