Matukio :Balozi Seif Ali Aongoza wadau wa Habari kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Zanzibar - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Wednesday, 3 May 2017

Matukio :Balozi Seif Ali Aongoza wadau wa Habari kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Zanzibar






Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na wadau wa Habari kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani hapo katika Chuo cha Habari Kilimani Mjini Zanzibar. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud, Katibu Mtendaji Baraza la Habari Tanzania Bw. Kajubi Mukajanga, kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Chuo cha Habari Zanzibar Nd. Chande Omar na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo anayesimamia Habari Nd. Hassan Mitawi.

Mkuu wa Chuo cha Habari Zanzibar Nd. Chande Omar Omar akitoa ufafanuzi juu ya Umuhimu wa Wanahabri kuzingatia suala la Amani katika uandishi wao wa kila siku.

Viongozi wa Meza Kuu kutoka kulia Katibu Mtendaji wa MCT Bw. Kajubi Mukajanga, Mkuu wa Mkoa Mjini Maghribi Mh. Ayoub, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif, Mkuu wa Chuo cha Habari Zanzibar Nd. Chande na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Nd. Hassan Mitawi wakifuatilia hafla ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari hapo Kilimani.

Kikundi cha Utamaduni cha Mkoa Mjini Magharibi kilitoa Burdani katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari hapo katika Ukumbi wa Chuo cha Habari Kilimani Mjini Zanzibar.

Katibu Mtendaji Baraza la Habari Tanzania Bw. Kajubi Mukajanga akitoa salamu kwenye hafla ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani Mjini Zanzibar.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo anayesimamia Habari Nd. Hassan Abdulla Hassan Mitawi akifafanua jambo kwenye maadhmisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Dunani.

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mheshimiwa Ayoub Mohamed Mahmoud akijiandaa kumkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari yaliyofanyika katika Viunga vya Chuo cha Habari Zanzibar kiliopo Kilimani Mjini Zanzibar.



Washiriki mbali mbali waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani yaliyofanyika katika chuo cha Habari Zanzibar kilipo Mtaa wa Kilimani.

Balozi Seif Ali Iddi kati kati waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Taasisi mbali mbali za Habari Nchini mara baada ya kufungua mdahalo wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud, Katibu Mtendaji Baraza la Habari Tanzania Bw. Kajubi Mukajanga, kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Chuo cha Habari Zanzibar Nd. Chande Omar na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo anayesimamia Habari Nd. Hassan Mitawi. Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment