Na Faustine Ruta, Bukoba
Ligi Kuu Vodacom imeendelea tena Jumamosi na katika Uwanja wa Kaitaba tukishuhudia Timu ya Kagera Sugar ikitoka sare tasa ya 0-0 dhidi ya Timu ya JKT Ruvu inayoshikilia nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa Ligi kuu Vodacom msimu huu.
Kikosi cha Timu ya JKT Ruvu kinachonolewa na Kocha wa zamani wa Simba, Kagera Sugar, Ashanti United na sasa JKT Ruvu King Kibadeni' kilionekana kukosa mbinu kuifunga Timu ya Kagera Sugar kipindi cha pili baada ya kuonekana kuwa na nguvu kwa kuingiza wachezaji waliokuwa na kasi kubwa.
Kagera Sugar nao walikuwa wakifanya mashambulizi ya kila mara lakini hawakuweza kupata bao lolote kwenye jitihada zao zote hizo za kipindi cha kwanza na cha pili. Hadi kipindi cha pili kinalizika dakika 90 hakuna timu iliyoweza kumfunga mwenzake.
Kocha wa zamani wa Simba, Kagera Sugar/Ashanti United/ Abdallah King Kibadeni(kushoto) akiteteta jambo na Viongozi wa Timu ya Kagera Sugar mtanange ulipomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Kagera Sugar imetoka sare ya 0-0 na Timu ya JKT Ruvu.
No comments:
Post a Comment