Matukio : Balozi Dk. Asha-Rose Migiro Ahudhuria Uzinduzi wa WASATU Northampton, Uingereza - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Sunday, 9 April 2017

Matukio : Balozi Dk. Asha-Rose Migiro Ahudhuria Uzinduzi wa WASATU Northampton, Uingereza


Na Freddy Macha


Jumuiya ya wasanii Watanzania Uingereza (WASATU) ilizunduliwa kwa vigelegele na muziki mjini Northampton , katikati ya Uingereza jumamosi iliyopita. Tafrija hiyo ndogo lakini iliyowakutanisha zaidi ya Watanzania mia moja na marafiki zao wa Kenya, Uganda, Kongo , Nigeria, Uingereza nk, ilihudhuriwa na Mheshimiwa Balozi Dk Asha Rose Migiro. WASATU ilibuniwa mwaka jana kati ya wasanii wakiongozwa na mwanamuziki na mcheza sarakasi Fab Moses na promota wa vyakula vya Kitanzania, Bi Neema Kitilya. Asilimia 20 ya kipato cha onesho zilitolewa na WASATU kwa waliofikwa maafa ya mafuriko ya maji karibuni Tanzania. Watanzania na marafiki zao wakijimwaga ukumbi wa The Eastern District Social Club, Northampton.
Furaha na shangwe ya WASATU Balozi Migiro (katikati) na mwana WASATU- mcheza ngoma asilia, Khadija Ismail. Wa kwanza ni Mtanzania, Salma Kashinde Muziki motomoto, Northampton
Bango la shughuli Balozi Migiro akihutubia tafrija Mpiga sasafoni mkongwe na mwanaWASATU- RamaSax- mzawa wa Tanga akipuliza vituz WASATU. Toka kushoto nyuma, Rama Sax, Saidi Kanda, John Londo, Fab Moses , Freddy Macha Mbele : Khadija Ismail na Neema Kitilya. Picha na Shah Vitumbua vya Neema Kitilya Nyama Choma Mwana WASATU Fab Moses akionesha vituko vyake vya Sarakasi Mwanamuziki wa Kikongo aliyehamia Tanzania miaka mingi, Kawele Mutimanwa na bendi ya “Afrika Jambo” jukwaani Northampton Mwanamuziki mlemavu na msanifu picha, Kea , toka Kenya aliyetengeneza tangazo la WASATU Mwanamuziki wa Kikongo Mboka Lia ( anayejulikana kwa jina “Burkina Faso”) ndani ya nyuzi na sakata sakata la WASATU

Mwanamuziki mlemavu aliyekomaa- mtunzi, mwimbaji na mpiga gitaa hatari, John Londo – mwana WASATU aliyebobea. Kileleni Northampton bila kukosa.

No comments:

Post a Comment