Michezo : Burundi U17 Wapasha Asubuhi hii Kaitaba , Jioni Kumenyana na Wenyeji Serengeti Boys - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 30 March 2017

Michezo : Burundi U17 Wapasha Asubuhi hii Kaitaba , Jioni Kumenyana na Wenyeji Serengeti Boys


Na Faustine Ruta, Bukoba




Timu ya Vijana U17 ya Burudi leo asubuhi imefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Kaitaba kujiweka kisawasawa na kuusoma uwanja huo ili kujiimarisha vyema kabla ya kukutana uso kwa uso leo na Timu ya Tanzania ya vijana wenye umri wa miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys. Timu hii itacheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani hapa Kagera. Timu hii itacheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani hapa Kagera. Mchezo wa kwanza utaanza kuchezwa leo hii Machi 30, 2017 na kurudiana Aprili mosi, mwaka huu. Hata hivyo Mvua iliweza kunyesha na kukatisha zoezi lao asubuhi na hatimae kurudi kwenye makazi waliyofikia jana baada ya kuchelewa kufika Bukoba na kutoweza kufanya mazoezi kwenye uwanja huo.

Nayo Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya vijana wenye umri wa miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys jana Jamatano walifanya mazoezi asubuhi saa nne kujiweka tayari na mchezo wao wa leo na Timu hii ya Burundi.

Serengeti Boys itakuwa kambini mjini hapa Bukoba hadi Aprili 2, mwaka huu ambako Serengeti Boys ambayo inajiandaa na michuano Afrika huko Gabon itarejea Dar es Salaam Aprili 2, mwaka huu ambako imepangwa kucheza na Ghana Aprili 3, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo utatanguliwa na hafla ya kuagwa kwa kukabidhiwa bendera.

Vijana wa Burundi wakiwa wanateta jambo na kufurahia Uwanja huo wa Kaitaba asubuhi hii ambako wanataraji kupambana na Serengeti Boys leo hii kwenye mchezo wa kwanza wa Kirafiki wa Kimataifa. Pia watarudiana siku ya Jumamosi.





Timu hii itacheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani hapa Kagera. Mchezo wa kwanza utaanza kuchezwa leo hii Machi 30, 2017 na kurudiana Aprili mosi.









Viongozi wa Timu hiyo yaBurundi wakiwaangalia kwa Makini Vijana wao ambako mapaka tunatoka kwenye Uwanja huo tuliweza kupata habari kuwa hakuna mchezaji hata mmoja ambaye ameumia au ana jeraha la kuweza kumfanye awe nje ya Uwanja, Wote wako fiti kwa Mchezo wa leo dhidi ya Serengeti Boys.





Mvua kubwa ilinyesha na kukatisha Tizi lao kwenye Uwanja huo wa Kaitaba asubuhi hii na kwenda jukwaa kuu




Wakisikilizia Mvua...

No comments:

Post a Comment