Matukio : DC Chongolo Aongoza Oparesheni ya Kuteketeza Mashamba ya Bhangi , Longido Arusha - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 30 March 2017

Matukio : DC Chongolo Aongoza Oparesheni ya Kuteketeza Mashamba ya Bhangi , Longido Arusha


Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Longido ikiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Godfrey Daniel Chongolo imeendelea na oparesheni ya kuteketeza madawa ya kulevya katika kata ya Lang'atadabash wilayani humo. Jumla ya mashamba yenye ukubwa wa ekari 5 yaliyokuwa yamelimwa bangi yameteketezwa.

Sehemu ya Bhangi ikichomwa moto,kuhakikisha haichuliwi tena kwa matumizi mengine ya ulevi.

Mkuu wa wilaya ya Longido,Godfrey Daniel Chongolo akijiandaa kuanza kuongoza oparesheni ya kuteketeza dawa za kulevya aina ya Bhangi akishirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama katika kata ya Lang'atadabash wilayani humo. Jumla ya mashamba yenye ukubwa wa ekari 5 yaliyokuwa yamelimwa bangi yameteketezwa.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya pamoja na DC wa wilaya ya Longido,Mh Daniel Chongol ( pichani kulia) wakiendelea na oparesheni ya kuteketeza dawa za kulevya aina ya bhangi katika kata ya Lang'atadabash wilayani humo mkoani Arusha

No comments:

Post a Comment