Na Betty Alex, Arusha
Chama cha mawakili Tanganyika (Tanganyika Law Society) kinatarajia kufanya uchaguzi mkuu wa urais wa chama hicho kesho ambapo hadi sasa wagombea watano wamejitokeza kugombea nafasi hiyo.
Akizungumza katika mkutano mkuu wa chama hicho unaoendelea jijini Arusha rais mstaafu anayemaliza muda wake John Seka amesema uchaguzi wa mwaka huu umekua na hamasa kwakuwa umehusisha wagombea ambao wanafahamika zaidi na jamii na pia umefanyika kwenye sheria mpya za uchaguzi wa chama.
Seka amewataja wagombea hao maarufu kuwa ni Tundu Lisu,Fransis Stola,Laurence Masha,Victoroia Mandarin na Godwin Mwapongo.
Aidha Seka amewataka wanasheria kuzingatia misingi ikiwa ni pamoja na kuisaidia na kuishauri serikali katika utungaji wa sheria za bunge na mahakama na ili kuongeza nguvu katika kuwasaidia wanyonge na wasio na uwezo waweze kupata haki.
Amewataka wanachama wa chama hicho kujitathimini ni kiongozi gani atakayefaa kupigiwa kura ili aweze kukabidhiwa kijiti cha kuongoza chama hicho.
Kwa upande wake wakili wa kujitegemea Dk. Eva Hawa Sanare amewataka wanasheria kusoma sheria mpya ya katiba ya Kenya law society kwa kuwa wanasheria bado hawajaelewa utawala wa sheria Wajiendeleze ili kuepuka kesi ambazo hazijakamilika kwani baadhi yao wamekuwa wakiendesha kesi ambazo hazijakamilika Amesema kuwa bila wanasheria kufanya kazi yao na kuielewa kwa undani hawataweza kuendeleza majukumu yao ya kuisaidia jamii.
TLS ni Nini?
“The Tanganyika Law Society is the Bar association of Tanzania Mainland, founded in 1954 by an Act of Parliament – the Tanganyika Law Society Ordinance, Chapter 344 of the Laws.
No comments:
Post a Comment