Matukio : Wengi Wajitokeza Kumuaga Marehemu Amina Athuman, Jijini Dar es Salaam - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


17 Jan 2017

Matukio : Wengi Wajitokeza Kumuaga Marehemu Amina Athuman, Jijini Dar es Salaam



Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mwandishi wa Habari za Michezo wa Gazeti la Uhuru, Amina Athuman walipokuwa wakioutoa nyumbani kwake Banana, Dar es Salaam leo, kuliingiza kwenye gari tayari kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Lushoto kwa mazishi.

Mwili wa aliyekuwa Mwandishi wa Habari za Michezo wa Gazeti la Uhuru, marehemu Amina Athumani ukiombewa dua nyumbani kwake, Banana, Ukonga.

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania, Juma Pinto (kushoto) akimzungumzia marehemu Amina kuhusu uchapakazi wake enzi za uhai wake

Baadhi ya waombolezaji wakiwemo wanahabari wakiwa eneo la msiba nyumbani kwa marehemu Amina Athuman, Banana, Ukonga Dar es Salaam

Mwili ukpelekwa kwenye gari




Mhariri Msanifu Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, ambaye kabla ya kujiunga na gazeti hilo alikuwa Mhariri Mtendaji wa gazeti la Uhuru,Joseph Kulangwa (kushoto), na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania, Juma Pinto wakiwa na huzuni wakati jeneza lenye mwili wa Amina Athuma likitolewa ndani tayari kusafirishwa kwenda Lushoto.

Mume wa marehemu Amina, Towfiq Majaliwa

Ndugu wa marehemu

Kiongozi wa kundi la wasapu la Waandishi wa Habari za Michezo Innocent Okamwa (kulia) akimkabidhi Baba mkubwa wa marehemu Amina Athuman, Athuman Kazukamwe mchango wa rambirambi sh. 600,000 zilizochangwa na wanahabari wa kundi hilo.Katikati ni mwanachama wa kundi hilo, Somoye Ng'itu.

Kazukamwe akitoa shukrani kwa mchango huo




Sehemu ya waombolezaji

Mgane wa marehemu Amina, Towfiq Majaliwa akifarijiwa na Naibu Mhariri Mtendaji wa gazeti la Uhuru

Wanahabari wakiwa na huzuni.
(PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad