Matukio : RC Gambo apania kutokomeza vifo vya Mama na Mtoto Mkoani Arusha - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


6 Jan 2017

Matukio : RC Gambo apania kutokomeza vifo vya Mama na Mtoto Mkoani Arusha


Na Nteghenjwa Hosseah, Arusha


Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dokta Frida Mokiti amesema kuwa uhaba wa vituo vya afya katika maeneo ya pembezoni mwa miji umekua ukichangia vifo vya mama wajawazito na watoto kutokana na kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo.
Akizungumza katika Kikao kazi cha Mkoa kinachojadili hali ya afya ya mkoa, Dr. Mokiti amesema kuwa juhudi za makusudi zinahitajika kuhakikisha kuwa huduma za afya kwa mama na mtoto zinapatikana kwa urahisi ili kupunguza tatizo hilo ambalo limekua likirudisha nyuma afya ya wakina mama pamoja na kukatisha maisha yao.
Akizungumza katika Kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuhakikisha kuwa wanajenga Kituo cha Afya katika kila tarafa ili kusogeza karibu huduma za afya kwa wananchi pia amewataka viongozi kuweka mipaka katika maeneo ya zahanati ili kuepuka uvamizi wa maeneo hayo yanayowahudumia watu.


“Wakati sasa umefika wa kuhakikisha tunatokomeza kabisa changamoto hii ya vifo vya mama na mtoto, inasikitisha sana kuona mama anafariki wakati wa kujifungua kwa sababu tu amekosa huduma ya afya karibu na makazi yake,lazima tuwalinde na kuwajali wananwake, kwa sababu bila ya wao kujifungua hata sisi tusingekuwepo” Alisema Gambo.


Aliongeza kuwa Kila Halmashauri ihakikishe inatenga Fedha kwenye mapato yake ya ndani halkadhalika Ruzuku toka Serikali Kuu ielekezwe kwenye Miradi ya Afya na tuendelee kutafuta wadau watakaotusaidia katika utekelezaji wa miradi hii bila kusahau uhamasishaji wa nguvu za wananchi kwa Pamoja tutatokomeza tatizo hili.
Kwa upande wake Mkazi wa Arusha Hussein Igunge na Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Daniel Chongolo wameitaka serikali iboreshe huduma za afya ikiwemo upatikanaji wa madawa kwa wale waliokata bima ili waweze kunufaika na bima zao pamoja na uhaba wa watumishi katika sekta ya afya.

Post Top Ad