Waziri mkuu mstaafu na mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa amefanikiwa kufika katika eneo la Kaisho ambalo liko katika wilaya mpya ya Kyerwa mkoani Kagera.
Kaisho ni eneo linalopatikana kaskazini- Magharibi mwa wilaya ya Kyerwa ambapo upande wake wa magharibi ni kilometa chache kufikia mpaka wa Tanzania na Rwanda ambao ni pori la akiba la Ibanda na upande wake wa kaskazini pia ni kilometa chache sana kufikia mpaka wa Murongo ambao unatenganisha nchi ya Tanzania na uganda.
Aidha katika upande wake wa Mashariki, kaisho imepakana na pori la akiba la Rumanyika Orugundu.
Katika safari hiyo iliyojaa milima na mabonde, adha kubwa iliyosababishwa na ubovu wa barabara ambayo ilianzia katika mji wa bukoba majira ya saa nane mchana na kufika katika eneo hilo la Kaisho takribani majira ya saa moja usiku.
"Nawashukuruni sana kwa upendo wenu mlionionyesha na uvumilivu mkubwa wa kunisubiri mpaka nilipofika hapa kwenu, Mungu awabariki sana" alisema Lowassa.
Licha ya kumsubiri kwa muda mrefu sana, wakazi hao wa Kaisho na maeneo jirani wakiwa wamevalia sare zao za Chama cha Demokrasia na Maendeleo walikuwa wenye sura za furaha na bashasha nyingi wakimshukuru Lowassa kwa kuwakumbuka na kufika kwao.
No comments:
Post a Comment