Michezo : Taswira mbalimbali ya Simba ilivyoibamiza Yanga kwa Penati 4- 2 - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 13 January 2017

Michezo : Taswira mbalimbali ya Simba ilivyoibamiza Yanga kwa Penati 4- 2


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


NI AZAM VS SIMBA, klabu ya Simba imeendeleza ubabe kwa watani wao wa jadi Yanga baada ya kuwaondoa kwenye hatua ya nusu ya kombe la mapinduzi kwa mikwaju ya penati 4-2 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Amaan, Zanzibar.


Penalti za Simba zilifungwa na Nahodha Jonas Mkude, kipa Daniel Agyei, Muzamil Yassin na beki Mkongo Janvier Besala Bokungu, wakati kipa wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’ aliokoa mkwaju wa beki Mzimbabwe Method Mwanjali na kwa upande wa Yanga waliofunga penalti ni Simon Msuva na kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko wakati kipa Mghana wa Simba, Daniel Agyei aliokoa penalti za Dida na Mwinyi Hajji Mngwali.

Dakika 90 za mchezo huo zilianza kwa kasi kwa kila upande kutaka kuliona lango la mwenzake lakini umakini wa golikipa Daniel Aggey aliweza kudaka mpira uliopigwa na Haruna Niyonzima katika dakika ya nane na dakika ya 16, kiungo Mohammed Ibrahim alijaribu kwa kupiga shuti kali lililodakwa na kipa wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’.

Kwa ujumla timu zote zilishambuliana kwa zamu, lakini Yanga ndiyo waliomiliki mpira zaidi wakicheza kwenye eneo lao na kuvusha upande wa pili kwa mipira mirefu, hivyo kuwafanya viungo wa Simba muda mwingi wawe wazurulaji katikati ya Uwanja.




Kikosi cha Simba SC kilikuwa; ⁠⁠Daniel Agyei, Janvier Bokungu, MOhammed Hussein 'Tshabalala', Abdi Banda, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shiza Kichuya/Jamal Mnyate dk72, James Kotei, Juma Luizio/Pastory Athanas dk77, Muzamil Yassin na Mohamed Ibrahim/Laudit Mavugo dk85.


Yanga SC; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Andrew Vincent ‘Dante’, Kelvin Yondan, Saidi Juma ‘Makapu’, Simoni Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Haruna Niyonzima na Deusi Kaseke/Emmanuel Martin dk63
Wachezaji wa Yanga wakijipanga kwa ajili ya kona.

Mshambuliaji wa Simba Mohamed Ibrahim akigangwa baada ya kuumia wakati wa mchezo wa nusu fainali ya kombe la Mapinduzi Usiku katika uwanja wa Amani, SAimba wakifanikiwa kuingia hatua ya fainali baada ya kushinda kwa penati 4-.

Maohamed Ibrahim akimtoka beki wa Yanga wakati mchezo wa nusu fainali ya kombe la Mapinduzi ,Usiku katika uwanja wa Amani, SAimba wakifanikiwa kuingia hatua ya fainali baada ya kushinda kwa penati 4-2

Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo akijaribu kumtoka beki wa Yanga Haji Mwinyi kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la Mapinduzi ,Usiku katika uwanja wa Amani, SAimba wakifanikiwa kuingia hatua ya fainali baada ya kushinda kwa penati 4-2

No comments:

Post a Comment