Matukio : Naibu Waziri, Mavunde atembelea Miradi ya Vijana ,Mbozi Mkoani Songwe. - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


13 Jan 2017

Matukio : Naibu Waziri, Mavunde atembelea Miradi ya Vijana ,Mbozi Mkoani Songwe.



Mhe Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Athony Peter Mavunde wa tatu kushoto akionyeshwa na kupata maelekezo juu ya ufugaji wa Samaki na Msimamizi wa Kituo cha Maendeleo ya Vijana SASANDA Ndg. Martin kambisi wa Pili kushoto.

Mhe Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Athony Peter Mavunde akizungumza na Vijana wajasilia mali wakulima na wafugaji wanaopata Mafunzo juu ya kilimo bora na Ufugaji wa kisasa katika Kituo cha maendeleo ya Vijana SASANDA kilichopo Wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe.

Mhe Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Athony Peter Mavunde akikagua duka la dawa baridi Moja kati ya Mradi wa Vijana wa kikundi cha MELANAKO kilichopata Mkopo wa shiling Milion Saba toka Wizarani.

Mhe Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Athony Peter Mavunde akitazama bidhaa za ujasiliamali Asali pamoja na Dawa ya Kusafishia chooni vinavyo zalishwa na kikundi cha Vijana wajasilia mali MELANAKO kilichopo wilayani Mbozi mkoani Songwe.

Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe:Athony Peter Mavunde wa kwanza kulia akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya mbozi ambae pia ni kaimu Mkuu wa Mkoa wa Songwe mhe:John Palingo mara baada ya kuwasili Mkoani Songwe.

Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe:Athony Peter Mavunde wa pili kiushoto akiongozwa na Kaimu RAS wa Mkoa wa Songwe Ndg:Samwel Razaro kusalimiana na Watumishi mbalimbali wa serikali alipo wasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Songwe,

Kaimu Afisa Elimu wa Mkoa wa Songwe Ndg:Samwel Mshana akimsomea Mhe Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Athony Peter Mavunde Taarifa ya Maendeleo ya Mkoa wa Songwe alipo kutana na kuzungumza na watumishi Mbalimbali wa serikali mkoani Songwe.

Nawaomba Viongozi wa Halmashauri kwanza Ndani ya Halmashauri zetu mhakikishe mmetenga Maeneo ya Shughuli za kilimo kwa vijana, pili Kusimamia Urasimishwaji wa Saccos kwa kila Halmashauli, tatu Kusimamia kwa Uadilifu mkubwa juu ya Fedha za Mikopo kwa vijana kuhakikisha zinawafikia walengwa na Nne kwenda kasi katika utekelezaji wa Falsafa ya Serikali ya Awamu ya tano Juu ya Uchumi wa Viwanda”Aliyasema hayo Mhe Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Athony Peter Mavunde wakati akizungumza na Watumishi Mbali mbali wa Serikali Mkoani Songwe.

Mhe Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Athony Peter Mavunde akikagua Mradi wa Ufugaji wa Ng’ombe wa kisasa alipotembelea Kituo cha maendeleo ya Vijana SASANDA chenye vikundi vya vijana 12 vyenye jumla ya Vijana 200 wanaojifunza shughuli mbali mbali za kilimo na Ufugaji wa kisasa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad