Usalama Barabarani : Mabalozi wa Usalama Barabarani na Jeshi la Polisi Wazindua kampeni ya ABIRIA PAZA SAUTI ,Jijini Arusha - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


20 Dec 2016

Usalama Barabarani : Mabalozi wa Usalama Barabarani na Jeshi la Polisi Wazindua kampeni ya ABIRIA PAZA SAUTI ,Jijini Arusha



Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, Eng. Nuru Selemani akizungumza na vyombo vya habari Desemba 19,2016. wakati wa zoezi la ukaguzi wa vyombo vya usafiri na madereva pamoja na elimu kwa abiria kujua haki na wajibu wao wawapo safarini.
Kamanda Nuru ameeleza kuwa Jeshila Polisi limejipanga vizuri kuhakikisha kwamba wanadhibiti kikamilifu vyanzo vyote na uwezekano wa kutokea kwa ajali zinazozuilika hasa kipindi hiki cha simu wa sikukuu ambapo wasafiri huwa wengi. Akitoleamfano, amesema mapaka mwakahuu ukiwa unaelekea ukingoni, wameweza kudhibitikwa kiwango kikubwa ajali za mabasi ya abiria jambo ambalo limechangiwa na uamuzi wakuwafikisha maahakamani madereva wazembe tofauti na awali walipokuwa wakiwatoza tu nauli. Picha Zote na Seria Tumainiel


Mmoja wa madereva akipimwa iwango cha ulevi kuona yuko kwenye kiwango sahihi kuruhusiwa kuendelea na safari na abiria wake ama la. Zoezi hilo lilifanyika kwa madereva wenginani mmoja tu ndiye aliyepatikanaakiwana kiwango kikubwa cha ulevi na kuondolewa kwenye gari.



RTO Arusha, Eng Nuru Selemani akishuka kutoka kwenye gari baada ya kufanya ukaguzi


Kamanda kwa Kikosi cha usalama Barabarani Eng Nuru Selemai(katikati) akifafanua jambo kwa vijana wake



Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, Eg. Nuru Selemani akielekeza masuala mablimbali na kujibu maswali ya abiria na wasafirishaji katika eneola Stand Kuu ya mabasi Arusha Desemba 19, 2016
.

Mabalozi wa Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha wakiwa eneola standakuu ya Mabasi yanayotoka nje ya Arusha mapemaleo asubuhi katika pilikapilika za kuendesha zoezilakutoa elimu kwa abiria kuhusiana na masualammbalimbali ya wajibu na haki za abiria kwa lengola kuhakikisha safari inakuwa salama. Kutoka kushotoni makamu Mwenyekiti Bakari Msangi anafuatiwana Balozi Vero Ignatus na kisha Mweyekiti Stellah Rutaguza


Mmmoja wa wasafirishaji abiria akihojiwana waandishiwa habari na kuelezea baadhi ya changamotona kero wanazokutana nazo toka kwa abiria safarini ikiwemo malalamiko ya abiria kudhani garini bovu pale linapotembea kwa kikomo cha spidi 80 kwa saa. (80km/hr)


Mwenyekiti wa Mabalozi wa Usalama barabarani (RSA) Mkoa wa Arusha, Bi. Stellah Rutaguza akitoa ufafanuzi kwa mwakilishi wa wakata tiketi za abiria Stendi Kuu Arusha.


Makamu Mweyekiti wa RSA, BakariMsangi akifafanua jambo kwa wadau wa usafiri na usafirishaji






Baadhi ya picha za pamoja baina ya Askari wa usalama wa Barabarani na Mabalozi wa usalama Barabarani kutoka Taasisi ya kiraia ya RSA

 
Balozi wa RSA Vero Ignatus akishuka kwa tahadhari kutoka kwenye moja ya mabasi mara baada ya kutoa elimu na basi hilo kukaguliwa na kuruhusiwa kuondoka.

Post Top Ad