Matukio : Ndoa ya "Upepo" Hatimaye YafungwaRasmi Jijini Mbeya - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


24 Dec 2016

Matukio : Ndoa ya "Upepo" Hatimaye YafungwaRasmi Jijini Mbeya


Na JamiiMojaBlog,Mbeya

HATIMAYE lile tukio lililovuta hisia za watu wengi la bibi harusi, Given Mgaya, kukimbiwa kanisani na mchumba wake siku ya harusi, limepatiwa jibu baada ya bwana harusi , Samwel Mwakalobo, kujirudi na kuamua kutimiza ahadi yake ya kufunga ndoa.

Ndoa hiyo imefungwa leo majira ya saa tisa Desemba 23 katika Kanisa la (K.K.K.T) Usharika wa Isanga na kufungishwa na Mchungaji, Mathias Andangile Mwakijungu, huku tukio hilo likishuhudiwa na idadi kubwa ya waumini na wananchi wa kawaida waliojitokeza kanisani hapo.

Kabla ya maharusi hao kula kiapo cha ndoa, Mchungaji Mwaijungu alitumia zaidi ya saa moja kutoa nasaha kwa maharusi kutokana na tukio lilotokea Disemba 16 mwaka huu baada ya Bwana harusi kuingia mitini bila kutoa sababu zozote.

Mbali na kutoa nasaha kwa maharusi,pia Mchungaji Mwaijungu alitumia fursa hiyo kuwaonya baadhi ya waumini na watu wengine kuacha tabia ya kueleza mambo wasiyo yajua tena bila kuwa na uhakika.

Alisema tabia hiyo huenda ndiyo iliyosababisha tukio la kukwama kufungwa kwa ndoa hiyo baada ya baadhi waumini na watu wengine kwa maslahi yao waliamua kueneza uzushi ulioibua taaruki kubwa.


Baada ya nasaha hizo na kunukukuu baadhi ya vifungu ya maandiko Bibliatakatifuy ndipo ulipofika muda kwa maharusi hao kutimiza ahadi ya kula kiapo cha uaminifu katika ndoa yao.

Mara baada ya kufunga ndoa, akizungumza njeya kanisa na waandishi wa habari bwana harusi Mwakalobo aliwaomba radhi ndugu jamaa na marafiki na kwamba kilicho tokea ni mapito.

“Ndugu zangu nawathibitishia kuwa alipangalo Mungu binadamu hawezi kulitengua. Ni kweli tulipanga tarehe ile lakini sisi ni wanadamu Mungu alipanga. Ule ulikuwa ni upepo na ulipita. Niwaombe radhi ndugu jamaa namarafiki kwa hilo liliotokea” alisema Mwakalobo


Bibi harusi hakupenda kuzungumzia suala hilo kwa kusema kwamba lililotokea lilitokea na kila kitu anamwachia Mungu.
Bwanaharusi Ndugu Samwel Makalobo akivishwa pete ya ndoa na Mke wake Given Mgaya katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa Isanga jijini Mbeya .Picha na Keneth Ngelesi.

Bwanaharusi akisaini hati ya Ndoa mbele ya mchungaji wa kanisa hilo Ndugu Mathias Mwaijungu mara baada ya ndoa hiyo kufungwa rasmi Desemba 23 mwaka huu.

Bibi harusi akisaini hati ya Ndoa mbele ya mchungaji wa kanisa hilo Ndugu Mathias Mwaijungu mara baada ya ndoa hiyo kufungwa rasmi Desemba 23 mwaka huu.


Hapa ni baada ya kutangazwa rasmi kuwa mume na mke.

Bibi harusi akitabasamu kwa furaha baada ya kutoka kanisani

Bwana na bibi harusi wakitoka kanisani kwa chereko na vifijo

Maharusi wakiondoka kanisani

Post Top Ad