MKURUGENZI
Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi
Mramba, (mbele kulia), akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kufua
umeme wa gesi wa Kinyerezi II jijini Dar es Salaam
NA K-VIS BLOG/KAHLFAN SAID
MKURUGENZI
Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi
Mramba, (anayezungumza pichani), amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi
wa mradi wa umeme wa gesi wa Kinyerezi II utakaozalisha umeme wa
Megawati 240 unaotekelezwa na shirika hilo jijini Dares Salaam.
Mradi
huo ulizinduliwa Machi 2016 kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, kuweka jiwe la msingi ambapo
eneo hilo lilikuwa pori tu kazi ya kusafisha eneo ili kuanza ujenzi
ilianza mieziminane iliyopita.
“Kwa
wale waliokuwepo siku Mheshimiwa Rais anaweka jiwe la msingi la ujenzi
wa mradi huu, mtakumbuka kuwa eneo lote hili lilikuwa pori, napenda
niwapongeze wahandisina mafundiwote mnaotekeleza ujenzi huu kwa kazi
nzuri nakasi ya kuridhisha.” Alipongeza Mhandisi Mramba, ambaye
alitembelea eneo hilo mwishoni mwa wiki kukagua maendeleoyaujenzi wake.
Wahandisi
wa TANESCO wakishirikiana na wenzao kutoka SUMITOMO CORPORATION NA
TOSHIBA za Japan na washauri wa mradi Lahmeyer International ya Humburg
nchini Ujerumani, ndio wanaojenga mitambo hiyo kwa ambapo unatekelezwa
kwa fedha za walipa kodi wa Tanzania na Japan.
Akitoa
taarifa ya maendeleo ya ujenzi huo, Meneja Mradi, Mhandisi Stephen
Manda alisema ni pamoja na ujenzi wa msingi wa kitalu namba moja
(Foundation Works Block I na ujenzi wa msingi watenki la kuhifadhia maji
(raw water tank).
“Kazi
inaendelea vizuri napenda kukujulisha kuwa baadhi ya vifaa muhimu
vimekwisha wasili na tunachosubiri pengine kufikia mwezi Januari ni
kuwasili kwa mashine zenyewe (Turbines), hivi sasa tuko kwenye
mazungumzo na watu wa TANROAD na mamlaka nyingine kuhusu utaratibu wa
kusafirisha mitambo hiyo kutoka bandarini kuiletahapa.” Alifafanua
Mhandisi Manda.
Akielezea
zaidi kuhusu manufaa ya mradi huo pindi utakapokamilika, Mkurugenzi
Mtendaji wa TANESCO, Mhanidis Felchesmi Mramba alisema, TANESCO
iliwaahidi watanzania kuwa kwa kushirikiana na serikali itaendelea
kuboresha miundombinu ya umeme ikiwa ni pamoja na kuzalisha umeme mwingi
zaidi ili hatimaye uende sambamba na malengo ya serikali yaawamu ya
Tano ambayo imedhamiria kujenga nchi ya viwanda.
“Nia
yan Mheshimiwa rais ya kujenga nchi ya viwanda itafanikiwa kwa vile
sasa umeme mwingi na wa uhakika utapatikana ili kuhudumia viwanda
vilivyopo na vipyavinavyoendelea kujengwa.”Alihitimisha Mhandisi Mramba.
Mhandisi Mramba, (kulia), akiongozana na Meneja Mradi wa ujenzi wa Kinyerezi II, Mhandisi Stephen Manda.
Ujenzi wa msingi wa tenki la kuhifadhia maji (raw water tank).
Ujenziwa msingi wa moja ya sakafu ya kufunga mashine za kufua umeme, (Foundation work block).
Mhandisi Manda, (kulia), akifafanua masuala mbalimbali yahusuyo maendeleo ya ujenzi huo
Mhandisi Manda akiwasilisha taarifa ya hatua mbalimbali za ujenzi wa mradi huo.
Jengo la muda la utawala.
Kazi ya kuhamisha kifusi ikiendelea
Mhandisi Manda aakionyesha kitu.
Meneja
Mwandamizi wa TANESCO anayeshughulikia miradi ya usafirishaji na
usambazaji umeme, Mhandisi Gregory Chegere (kulia), akizungumza jambo na
mmoja wa Wahandisi viongozi kutoka kampuni ya TOSHIBA ya Japan.
"Mambo
swafi" ndivyo anavyoonekana akisema, Mhandisi Mramba, wakati akianza
ukaguzi wa mradi huo akifuatana na Meenja Mradi, Mhandisi Manda
(kushoto).
Mameneja na maafisa wa TANESCO waliofuatana na Mkurugenzi Mtendaji kutembelea eneo hilo.
Mhandisi kiongozi wa kampuni ya TOSHIBA.
Mameneja na maafisa wa TANESCO.
No comments:
Post a Comment