Mkuu
wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo akiwahutubia wajasiriamali
hawapo pichani wakati wa sherehe za ufungaji wa maonyesho ya tisa kanda
ya mashariki yaliyofanyika katika viwanja vya mwanakalenge Wilayani
Bagamoyo.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
mmoja
wa wajasiriamali walioshiriki katika maonyesho ya tisa ya kanda ya
mashariki yaliyofanyika katika viwanja vya mwanakalenge Wilayani Bgamoyo
Jacob Luis akiwa katika gari yake ambayo ameitengeneza yeye mwenyewe
ambapo mpaka kukamilika kwake ametumia gharama ya kiasi cha shilingi
milioni tisa .(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO
WAJASIRIAMALI
nchini wametakiwa kuhakikisha wanakuwa wabunifu na kutengeneza bidhaa
zenye ubora wa kiwango cha juu ili kuweza kuleta ushindani na kuzipeleka
katika soko la afrika mashariki ambalo lina idadi kubwa ya watu ili
ziweze kuuzika na kukuza pato la Taifa.
Kauli
hiyo imetolewa na MKUU wa Mkoa wa Pwani Injnia Evarist Ndikilo wakati wa
sherehe za ufungaji wa maonyesho ya 9 ya wajasiriamali wadogo wadogo
kutoka kanda ya mashariki yaliyofanyika katika viwanja vya Mwanakalenge
Wilayani Bagamoyo.
Ndikilo
alisema kwamba ili bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali wa
Tannzania ziweze kuuzika katika soka la afrika mashariki kunahitajika
juhudi za makusudi kutoka kw amamalaka ya chakula na dawa (TFDA) pamoja
na Shirika la viwango Tanzania (TBS) kuzingatia maagizo waliyopatiwa na
serikali wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo ili kuweza kukuza uchumi
wa nchi.
Ndikilo
akizungumzia kuhusina na changamoto inayowakabili wajasiriamali hao
katika suala la upatikanaji wa vifungashio katika kuhifadhi bidhaa zao
amesema kwamba serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya viwanda na
biashara ipo tayari kutoa fungu la fedha kwa ajili ya kuweza kuwa na
vifungashio hapa nchini kuliko kuviagizia kutoka nje ya nchi kwani ni
gharama kubwa.
“Kwa
upande wangu mimi napenda kuchukua fursa hii ya kuwaomba wajasiiamali
kuwa wabunifu katika bidhaa ili kuweza kuleta ushindani mkubwa katika
soka la afrika mashariki kwani kule ndio kuna idadi ya watu wengi zaidi
kwa hivyo mkilizingatia hilo kutaweza kuleta mabadiliko chanya ya kuleta
maendeleo,”alisema Ndikilo.
Aidha
Ndikilo aliwataka wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wote nchini kuhakikisha
wanatenga maeneo maaalumu kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo vidogo
na vikubwa ambayo vitaweza kusaidia kwa kisi kikubwa kuwapatia ajira
vijana ambao wengi wao hawana kazi za kufanya.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa shirika la viwanda vidogovidogo (SIDO)
Tanzania Profesa Syvester Mpanduji alibanisha kwamba maonyesho hayo
yameweza kuwapa fursa wajasiriamali kubadilishana ujuzi kupata mafunzo
ikiwemo pamoja na kukuza uchumi wao kutokana na kuuza bidhaa zao .
Nao
baadhi ya washiriki katika maonyesho hayo akiwemo Jacob Luis, Jania
Omary pamoja na Rehema John walisema kwa sasa wanakabiliwa na chngamoto
kubwa ya kutokuwa na vifungashio maalumu kwa ajii ya bidhaa zao hivyo
wameimba serikali kupitia wizara ya viwanda na biashara kuwasaidia ili
kuweza kufikia malengo yao.
MAONYESHO
hayo ya kanda ya mashariki ambayo yamefungwa rasmi na mKuu wa Mkoa wa
Pwani yameandaliwa na shirika la viwanda vidodovidogo (SIDO) Tanzania na
yamewashirikisha wajasiriamali wadogo wadogo na wale wa kati zaidi ya
200 kutoka mikoa mitano ya Dar es Salaam, morogoro, Lindi, Mtwara ,
pamoja na wenyeji Mkoa wa Pwani .
No comments:
Post a Comment