Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira (katikati katika
Ziara ya Mgodi wa Dhahabu wa Bulyankulu Wilayani Kahama. (Picha na
Evelyn Mkokoi wa OMR.
Evelyn Mkokoi na Anceth Nyahore - Kahama
SIKU moja baada ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muugano
Mazingira Luhaga Mpina, kubaini ukiukwaji mkubwa wa usimamizi wa sheria
za Mazingira na Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) kuiadhibu kulipa
faini ya shilingi milioni 15, jana Naibu Waziri huyo amebaini umwagaji
wa maji taka ovyo katika dampo la tala la Busoka mjini hapa.
Naibu waziri huyo katika ziara yake ya siku ya pili yenye staili ya
kushitukiza na kuachana na ratiba aliyopangiwa, alishuhudia uchafuzi
wa mazigira wa gari moja aina la Fuso lenye namba za usajili T 245 BHC
linalomilikiwa na Shule ya Msingi ya Kwema ya mjini Kahama lililokuwa
likiendeshwa na Johanas Mwambeya,likimwaga maji taka kando ya barabra
karibu na dampo hilo.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina
katika Ziara ya kukagua DAMPO la Majitaka Mjini Kahama akionyesha namna
ambavyo maji taka yanayomwagwa kiholela yalivyoenea kwa wingi katika
eneo la karibu na barabara.
Naibu Waziri huyo, aliyekuwa amefauatana na Wakaguzi wa Mratibu wa
NEMC kanda ya Ziwa,Jamal Baruti, alisema kitendo hicho ni hujuma
katika mazingira na ukiukwaji wa kifungu namba 187 cha utunzaji wa
mazingira na kuagiza halmashauri hiyo ndani ya siku saba iwe imechimba
bwawa maalum kwa ajili ya kumwaga maji taka na kutoa adhabu ya mmliki
wa gari hilo kulipa shilingi milioni 1.2 ambazo mmiliki huyo alilipa
mara moja..
“Ni jana tu adhabu ya shilingi milioni 15 imetolewa kwa halmashauri ya mji wa
Kahama kwa ukiukwaji wa usimamizi wa sheria za utunzaji mazingira, na
leo tunashuhudia uchafuzi mkubwa…..tumepita maeneo mengi hatujaona
hali hii ya umwagaji vinyesi tena kando ya barabara na ni mchana
kweupe….umwagaji katika eneo hilo la tambalare kuelekea katika vyanzo
vya maji inasikitisha kweli kweli”Alisema Mpina.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Luhaga Mpina
(kushoto) akiwa na wataalam katikati ni Bw. Jamali Baruti kutoka Baraza
la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ( NEMC) kanda ya ziwa na
Kulia ni Mwanasheria wa Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abraham Mdee
wakijadili jambo katika siku ya Pili ya Ziara Na Naibu Waziri Mjini
Kahama.
“Hali hii inatafasiriwa kuwa halmashauri au serikali hii ndiyo
inayowapelekea wananchi wake magonjwa ya kuambukizwa kama kipindupindu
na
Typhoid…..huduma nzuri zinazo tolewa na serikali kwa wananchi wake
sasa kwa mlango wa nyuma zinarudia wananchi kwa kuwaumiza….hili
haliwezekani,hakika Mkurugenzi Kahama hili limeonyesha uzembe mkubwa
katika kusimamia usafi wa mazingira na huu sio watumishi wadogo ni
wewe”Alisema Naibu Waziri huyo.
Naibu waziri huyo alisema kuwa hali hiyo imekuwa ikisababisha
uchafuzi mkubwa wa mazingira na hasa mkutitirisha maji machafu yenye
kinyesi katika vyanzo vya maji vilivyo karibu na maeneo ya dampo hilo.
Alisema na kuagiza kuwa mara tu baada ya kumaliza ziara yake ya siku
mbili wilayani Kahama angependa kusikia na kupata taarifa ndani ya
siku saba kuwa tayari bwawa maalum linachimbwa kwa ajili ya kumwaga
maji machafu.
Gari
la Kuzolea majitaka no T245 BHC mali ya shule ya kwema ya mjini Kahama
lililokamatwa likimwaga maji taka katika eneo la barabarani lisilo rasmi
leo ambapo Dereva wa gari hilo Bwana Thomas Mwambeya pamoja na kutozwa
faini ya shi milioni 1.2 likamatwa na kufishwa katika kituo cha police
cha Mjini Kahama.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo, ameiagiza halmashauri hiyo
kuacha mara moja kutupa taka katika uwanja wa wazi maarufu kama uwanja
wa Magufuri uliopo eneo la Majengo mjini Kahama, na kuwa taka zote
zilizopo ziondolewe na eneo la uwanja huo kuwa safi.
Kufuatia hali hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya mji wa Kahama
Anderson Msumba,aliahidi kutekeleza agizo la Niabu Waziri huyo, huku
akichukua hatua za kinidhamu za kuwasimamisha kazi baadhi ya maafisa
katika ofisi yake kwa kile alichodai kuwa wakati hali hiyo ikitokea
yeye alikuwa mapumzikoni katika likizo fupi.
Mabwawa
ya Maji Taka ya Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu Mjini Kahama uliojengwa
kitaalam na ado umekuwa ukilalamikiwa na wananchi wa vijiji jirani kuwa
katika msimu wa mvua mabwawa hayo yanajaa maji yenye sumu na kumwagika
katika mashamba ya wakazi hayo hivyo kuhatarisha maisha ya wakazi hao ,
mazingira na viumbe hai wengine.
Maafisa waliosimamisha kazi ni Mkuu wa Idara ya Usafishaji na
Mazingira,Martin Masele,Afisa Afya na Mazingira Johaness Mwabesi na
Deogratias Dotto Afisa Afya.
Naibu
Waziri mpina Pia alitembelea Mgodi wa kuzalisha Dhahabu wa Bulyankulu
uliyopo Kahama na kujionea hali ya mazingira mgoni hapo Pamoja na
kukagua mabwawa ya kisasa ya kuhifadhi maji taka yatokanayo na
uzalishaji kiwandani hapo Mgodi umekuwa ukilalamikiwa na wakazi vya
vijiji jirani kuwa wakati wa kipindi cha mvua mabwawa hayo hujaa maji na
kwenda kwenye eneo la makazi ya watu na mazingira.
Naibu
Waziri Mpina amelitaka Baraza la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa
Mazingira NEMC Kujiridhisha malalamiko hayo ya wananchi na kuagiza
uongozi wa mgidi kuchukua hatua stahiki pamoja na kurekebisha mapungufu
hayo iwapo yatabainika.