Na FK Blog- Kigoma,
MKUU wa Wilaya ya Kasulu Kanali Martin Mkisi
ameeleza kukerwa na tabia ya wakulima na wafugaji wanaovamia hifadhi ya Msitu
wa Kagerankanda na kufanya shughuli za ufugaji na kilimo katika msitu huo wenye
sifa pekee ya Uoto wa Asili Mkoani Kigoma.
Kauli hiyo aliitoa mwishoni mwa wiki katika
kikao cha Baraza la madiwani kilichokuwa kikiwasilisha taarifa mbalimbali za
utendaji kazi wa kamati husika katika kipindi cha Julai-Septemba
2016, ambapo mkuu huyo wa Wilaya alitumia nafasi hiyo kuwaasa madiwani wahamasishe
wananchi wapishe hifadhi hiyo kabla ya kutumika nguvu ya ziada.
Kanali Mkisi alisema changamoto ya
uvamizi katika msitu huo ni ya muda mrefu na kueleza kusikitiswa na vitendo
hivyo kutokana na kuwa vitendo hivyo ni janga kwa kizazi cha kijacho, kutokana
na makundi ya wakulima na wafugaji kuendelea kujazana katika msituni huo kwa
shughuli za kilimo na ufugaji wakati kuna maeneo makubwa yapo wazi na yana
rutuba kwa uzalishaji wa bidhaa zao.
“mimi ni kanali siendeshi wilaya kiraia ,nataka
sheria,kanuni na taratibu zitumike katika kurasimisha makazi si kuvamia misitu
ya asili yenye hadhi ya uoto wa asili na mimi niseme ukweli, nashangzwa na
baadhi ya viongozi wanalifumbia macho wakati rasilimali inatumiwa hovyo kwa
maslahi yenu binafsi” alisema
Aidha Mkisi alisema, hatojali zengwe
kwa kuwa amechaguliwa na serikali hivyo nitasimamia sheria, kanuni na taratibu
husika, na kusema kuwa aliondolewa katika nafasi yake huku akiwa
anasimamia sheria na kanuni hatosita kuendelea na shughuli nyingine.
Akizungumzia kero ya uvamizi wa hifadhi hiyo
Diwani wa kata ya Kagerankanda Ezekieli Mshingo, alikiri wananchi kutumia msitu
huo kwa zaidi ya miaka 12 kama kichaka cha wahamiaji haramu,ufichwaji wa silaha
haramu za moto pamoja na makundi ya wafugaji na wakulima kuongezeka kila
kukicha.
Mshingo alisema uvamizi unatokana na usimamizi
mbovu kuanzia ngazi ya juu hadi ya chini na kitendo cha kuwaondoa makundi hayo
katika msitu wa kagerankanda ni changamoto kwa kuwa, wavamizi wengi wanasaidiwa
na watu wakubwa hali inayochangia mauwaji kila mwaka na
kutolea mfano wa Novemba 3, 2016 kuna mfugaji mmoja Majigwa
Magesa ameuwawa na mwishoni na kwamba hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya
waharifu.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Wilaya ya Kasulu vijijini Yohana Mshita alisema taifa lilipofikia linahitaji
kiongozi muwazi, mkweli mwenye moyo wa dhati katika kuondoa kero za
wananchi kwa uadilifu huku akifuata sheria zilizopo lengo lkiwa ni kutimiza
malengo yake na kusema kuwa katika utendaji huo baadhi ya watendaji
wa halmashauri za wilaya wamekua na taba ya majungu ya kukwamisha utekelezaji
wa shughuli mbalimbali hivyo kumuomba mkuu huyo kutosikiliza maneno yao.
No comments:
Post a Comment