MKUU
wa wilaya ya momba Mkoani hapa,Juma Irando ametoa onyo kali kwa mganga
mtawala wa kituo cha afya cha Tunduma Dr Kaogo na kumtaka kujirekebisha
na kurekebisha mapungufu aliyobaini na kuwa tayari kuendana na kasi ya
Sereikali ya awamu ya tano na kuamtaka kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Hayo
aliyasema baada ya kwenda kutembelea kituo hicho cha afya jana na
kubaini utaratibu mbovu wa utoaji huduma zakiafya baada ya kukaa katika
kituo hicho kwa muda wa nusu saa bila ya kumuona hata muudumu mmoja
akiwa mapokezi
''Viongozi
niliongozana nao walilazimika kuwatafuta watoa huduma kwa dakika zaidi
ya 45 baada ya kuwasuburi mapokezi kwa kipindi cha dakika 30 bila kupewa
huduma pamoja na kuwepo kwa wagonjwa waliokuwa wakisuburi kusikilizwa
eneo la mapokezi kwa kipindi kirefu''alisema.
Hali
iliyomlazimu Dc Irando kuwasiliana na Mganga mkuu wa Wilaya ya Momba
aliyefahamika kwa jina moja Dr Felister na kumtaka ampe jina la mganga
mtawala wa kituo na mganga wa zamu, ambao walipatikana baada ya dakika
30 kinyume na utaratibu.alisema
Dc
Irando pia aligundua kutokujazwa kwa taarifa za wagonjwa katika vitabu
vya kuchukulia taarifa za wagonjwa kituoni hapo wakati akimuhoji mganga
mtawala wa kituo hicho aliyefahamika kwa jina la Dr Kaogo ofisini kwake,
ambapo vitabu vya wagonjwa vilivyokutwa kituoni hapo vilionyesha
kuhudumiwa wagonjwa 15 kwa siku na vingine kuonyeshwa kutokujazwa tangu
tarehe 11 mwezi huu.
''Nikiwa
kama mkuu wa wilaya siwezi kukubaliana nasuala la uzembe kazini ambaye
alisema uhalali wa kituo hicho kuhudumia wagonjwa 15 tu kwa siku licha
ya kuwa ndio kituo pekee kinachotoa huduma chenye hadhi ya
wilaya'',alisema baada ya kubaini kinaudumia wagonjwa kumi na tano.
Dc
Irando alipowahoji wagonjwa hao walikiri kutokusikilizwa kwa muda huo
hali iliyomlazimu mkuu wa wilaya kuwafata wahudumu wodini, kuonesha kuwa
hawakuwa wakijuwa uwepo wa Mkuu wa wilaya kituoni hapo, wauguzi
waliokutwa wodini hawakuonesha kushtuka wala kuuliza shida waliyonayo
hadi pale Dc Irando alipojitambulisha, huu ni ushahidi wa utaratibu
mbovu walionao watumishi wa kituo hicho kwa wagonjwa wanaofika
kuhudumiwa katika kituo chao.
Dc
alimtaka Mganga mkuu wa wilaya kumpa maelezo juu ya utaratibu mbovu wa
utoaji huduma kwa wananchi unaofanywa na watumishi wa kituo hicho pamoja
na kukaa na watumishi wa kituo hicho na kuwataka kubadilika mara moja
akiahidi kurejea hapo kesho yake.
Aliagiza
kuwepo kwa watoa huduma muda wote wa kazi na kutoa ovyo kali kwa mganga
mtawala wa kituo hicho Dr Kaogo na kumtaka kujirekebisha na kurekebisha
mapungufu aliyobaini na kuwa tayari kuendana na kasi ya Sereikali ya
awamu ya tano na kuamtaka kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
.Naye
Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Tunduma Ally Mwafongo (chadema)
alimwambia mkuu wa wilaya kuwa kituo hicho kina utaratibu mbovu na
watumishi wa kituo hicho wanafanya kazi kwa mazoea hivyo kumtaka mkuu wa
wilaya kuingilia kati ili wananchi wasiendelee kunyanyasika.
Akiongozea
juu ya huduma mbovu za watumishi wa kituo hicho Mwafongo alisema kuwa
alifika kituoni hapo siku kadhaa zilizopita mida ya saa mbili usiku
hakukuta wahudumu wala waganga wanaotakiwa kuwepo licha kukuta uwepo wa
wagonjwa waliokuwa wanasubiri kusikilizwa kwa muda mrefu na kumshukuru
mkuu wa wilaya kujionea yeye mwenyewe isijekuonekana kuwa wanawachongea
No comments:
Post a Comment