Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence
Museru leo amekutana na Balozi wa Cuba nchini Bwana Jorge Luis Lopez
Tormo na kufanya mazungumzo yenye lengo la kuomba kupatiwa wataalamu
waliobebea kwa ajili ya kutoa huduma za afya.
Katika
mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine Profesa Museru amemueleza
Balozi wa Cuba kwamba hospitali hiyo inatoa huduma za kibingwa, lakini
inakabiliwa na changamoto ya watalaam mbalimbali wakiwamo watalaam wa
wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU), usingizi, maabara na
Radiolojia.
Amesema
endapo watapatiwa watalaamu waliobobea kutoka Cuba watasaidia
kuwajengea uwezo wataalaam wa hospitali hiyo hivyo Hosptali ya Taifa
itaendelea kutoa huduma bora za kibingwa.
“Hii
ni Hospitali kubwa ya Taifa tunahudumia Watanzania wengi hivyo
tunahitaji ushirikiano wenu kwani tukipata watalaam hao itakua hatua
nzuri kwa kuwa watalaamu wetu watajifunza na kupata ujuzi na ndio maana
tunahitaji wale waliobobea,”amesema Profesa Museru.
Kwa
upande wake Balozi wa Cuba, Bwana Jorge Luis Lopez Tormo ameahidi
kuipatia muhimbili watalaamu waliobobea ili waweze kushirikiana na
watalaamu wa MHN katika kutoa huduma sanjari na kuwawezesha madaktari
na wataalamu wengine wa MNH kujifunza zaidi.
Balozi
huyo pia amepata fursa ya kutembelea baadhi ya Idara ikiwamo maabara
kuu, Radiolojia pamoja na Wadi namba moja ya wagonjwa wanaohitaji
uangalizi maalumu.
Balozi
wa Cuba nchini Tanzania, Jorge Luis Lopez Tormo akizungumza na
wakurungezi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) LEO katika mazungumzo
ya kuimarisha huduma za afya hospitali hapo. Kulia ni ofisa wa balozi
huo nchini Tanzania.
Baadhi
ya wakurugenzi wa hospitali hiyo wakimsikiliza Balozi wa Cuba, Jorge
Luis Lopez Tormo. Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili,
Profesa Lawrence Museru akiwa na wakurugenzi wenzake leo.
Wakurugenzi wakiwa kwenye mkutano huo Leo.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza kwenye mkutano huo Leo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Aminiel Agaesha akifafanua jambo kwenye mkutano.
Profesa Museru akimkaribisha balozi Tormo Leo katika hospitali hiyo.
Mkuu wa Idara ya Radiolojia, Dk. Flora Lwakatare akitoa maelezo jinsi mashine ya CT-Scan inavyotoa huduma kwa wagonjwa.
Balozi Tormo alipata nafasi ya kuitembelea wodi moja ambako wamelazwa wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu.
Mkurugenzi
wa Tiba Shirikishi katika hospitali hiyo, Dk Praxeda Ogweyo
akimtambulisha Mkuu wa Idara ya Maabara, Dk Alex Magesa kwa balozi huyo.
Balozi Jorge Luis Lopez Tormo akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi wa hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment