Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa Mh Job Masima
aliyeshinda kwa Senior akipiga mpira wakati wa mashindano ya PWC Trophy
yaliyofanyika Jumamosi Oktoba 22 katika uwanja wa Golf wa jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Lugalo Jijini Dar Es Salaam.
Baadhi
ya Watoto (Junior) wa Klabu ya Golf ya Lugalo walioshiriki mashindano
ya PWC Jumamosi Oktoba 22 Jijini Dar es Salaam wa Pili Kulia ni Mshindi
wa Kwanza wa Kundi hilo Almadius Simon wa Klabu ya Lugalo.
Wachezaji
wa Golf kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa Mh Job Masima, Dk Edmund Mndolwa aliyekuwa Mkuu wa majeshi
Jenerali Mstaafu George Waitara na Balozi Clemence Sanga wakibadilshana
mawazo kabla ya kuanza mashindando ya PWC yaliyofanyika Jumamosi Oktoba
22 katika Uwanja wa Golf Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Mshindi
wa Jumla wa mashindano ya PWC yaliyofanyika Jumamosi Oktoba 22 Jijini
Dar es Salaam Nicholous Chitanda wa Lugalo aliyeshika Vikombe akiwa
katika Picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa Kushoto ni mwenyekiti
wa Klabu ya Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo , wa kwanza kulia
ni Mwenyekiti wa TGU Joseph Tango na wa pili kulia ni Msuya Mkurugenzi
PWC .(Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ
Mchezaji
wa Klabu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo
Nicholous Chitanda imeibuka washindi wa Jumla katika mashindano ya wazi
ya PWC Trophy yaliyofanyika Jumamosi Oktoba 22 katika uwanja wa Golf wa
Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Chitanda
aliibuka na ushindi huo nakuwashinda wachezaji wengine zaidi ya 100
waliojitokeza kutoka Klabu zote Nchini baada ya kupata Mikwaju au Gross
74 huku kiwango chake cha Uchezaji kikiwa ni Tisa na hivyo kuibuka na
Mikwaju ya Jumla Net ya 65.
Katika
Division A ushindi ulinyakuliwa na Isack wanyenche kutoka Klabu ya
Arusha baada kupiga mikwaju 69 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni
Tatu na hivyo kuibuka na ushindi kwa kupiga mikwaju ya jumla 66 na
kufuatiwa na Juma Likuli wa Lugalo baada ya kupiga mikwaju ya jumla 68.
Kwa
upande wa Division B mshindi ni Dk James Legg wa Lugalo baada ya kupiga
mikwaju 84 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni 13 na hivyo kuwa na
mikwaju ya jumla 71 na kufuatiwa na Salum Mvita wa Dar es Salaam
Gymkhana kwa mikwaju ya Jumla 71.
Division
C kwa upande wake Mpiga Golf Reneir Kuhcmanu wa Lugalo aliibuka na
ushindi katika kundi hilo baada ya kupiga Mikwaju ya Jumla 68 huku
kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni 24 akifuatiwa na Kapten Amanzi
Mandengule wa Lugalo pia baada ya kupata mikwaju ya Jumla 69 huku
kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni 19.
Kwa
upande wa Kundi la Wazee ama Senior Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na
Jeshi la Kujenga Taifa Mh Job Masima alishinda kwa kupiga Mikwaju ya
Jumla 75 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni 18 akifuatiwa na
Balozi Clemence Sanga aliyepiga mikwaju ya Jumla 78 huku kiwango chake
cha Uchezaji kikiwa ni 16.
Wanawake
kwa upande wa kundi lao Chiku Elias wa Lugalo aliibuka na Ushindi kwa
Mikwaju ya JUmla 76 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni 10 na
kufuatiwa na Vicky Elias wa Lugalo kwa mikwaju ya Jumla 78 huku kiwango
chake cha uchezaji kikiwa ni Nane.
Katika
Upande wa Wachezaji wa Kulipwa Nuhu Mollel wa Arusha aliibuka Mshindi
,watoto Junior Almadious Simon wa Lugalo aliibuka na Ushindi baada ya
kupiga Mikwaju ya Jumla 70 na kwa upande wa Wachezaji wasaidizi au
Cardes Hendrick Nyenza wa Lugalo aliibuka Mshindi kwa Mikwaju 78
akifuatiwa na Deo Hassan wa Lugalo.
No comments:
Post a Comment