Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu Mhe. Jenista Muhagama (katikati) akikata utepe kufungua rasmi
maadhimisho ya Wiki ya Vijana , mkoani Simiyu. Kutoka kushoto ni
Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Anthony Mavunde, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Antony Mtaka (wa pili kutoka kushoto), Waziri Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Simiyu Titus Kamani na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Abdallah Possi (Mwenye Kofia).Picha na Aron Msigwa – NEC.
Wananchi wilayani Bariadi mkoani Simiyu wakipata elimu ya Mpiga Kura kwenye banda la Maonesho la NEC .
Na. Aron Msigwa –NEC.
9/10/2016. Bariadi –Simiyu.
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imepongezwa kwa kuanzisha programu
endelevu za utoaji wa Elimu ya Mpiga Kura kwa kuwafikia wananchi moja
kwa moja katika maeneo yao kote nchini.
Akitoa
pongezi hizo mara baada ya kutembelea Banda la Maonesho la Elimu ya
Mpiga Kura la NEC wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika
Bariadi mkoani Simiyu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Muhagama amesema
kuwa hatua ya NEC kutoa elimu ya mpiga kura kupitia maonesho hayo
inawasaidia wananchi kujifunza masuala mbalimbali kuhusiana na chaguzi
za Tanzania.
“
Nawapongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuanzisha utaratibu huu wa
kushiriki maonesho mbalimbali, mnafanya kazi nzuri, endeleeni hivyo
hivyo kuwaelimisha wananchi” Amesema Mhe. Jenista.
Ameeleza
kuwa ushiriki wa NEC katika maadhimisho ya Wiki ya Vijana unawapa fursa
vijana wengi kupata elimu sahihi kuhusu wajibu wao na majukumu ya Tume
ya Taifa ya Uchaguzi katika kuratibu na kusimamia Uchaguzi wa Rais,
Wabunge na Madiwani.
Kwa
upande wake Afisa Habari wa Idara ya Elimu ya Mpiga Kura ya NEC Bi.
Margareth Chambiri amwemweleza Waziri huyo kuwa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi imeanzisha program endelevu za kutoa elimu ya mpiga kura kwa
kuhakikisha kuwa wananchi moja kwa moja katika maeneo mbalimbali nchini.
Amesema
NEC inatoa elimu hiyo kwa wananchi ili kuwawezesha kuwa na uelewa
sahihi kuhusu utendaji wa Tume na masuala mbalimbali yanayohusu upigaji
wa kura, sheria, taratibu na kanuni zinazosimamia uchaguzi, taarifa za
wapiga kura na maelekezo ya namna ya kufanya endapo kadi zao za kupigia
kura zimepotea au kuharibika, mwananchi kuhama eneo moja kwenda jingine
kutokana na sababu mbalimbali.
Baadhi
ya wananchi waliolitembelea banda la NEC wameeleza kufurahishwa
ufafanuzi na elimu ya Mpiga kura inayoendelea kutolewa na Maofisa wa
Tume hiyo kupitia majibu ya maswali mbalimbali wanayouliza hususan
uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura kwa mujibu wa Sheria
ambao utakaowapa fursa ya kuhuisha taarifa zao pia kupewa elimu kuhusu
uendeshaji wa chaguzi mbalimbali hapa nchini.
Aidha, wameiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuendelea kutoa elimu ya Mpiga kura katika maeneo mengine nchini kwa ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi kupata elimu sahihi kuhusu utendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
No comments:
Post a Comment