Mkuu
wa gereza la Karanga, mjini Moshi, mkoa wa Kilimanjaro, ambako ndiko
kilipo kiwanda cha kutengeneza viatu, Kamishna Msaidizi wa Magereza,
(ACP), Hassan Bakari Mkwiche, (kushoto), akionyesha kitu, wakati
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, (wakwanza
kulia), alipotembelea kiwanda hicho ili kuona eneo lililotengwa kwa
ujenzi wa kiwanda kipya cha kisasa cha viatu, Oktoba 9, 2016. Wengine
pichani ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PPF, Steven Alfred, (wapili
kushoto), Mkuu wa magereza mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa
Polisi, (ACP), Anderson Kamtera.
Bw.
Erio, na maafisa wake, wakipatiwa maelezo na maafisa wa Jeshi la
Magereza alipokagua moja ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa
kiwanda hicho
NA K-VIS MEDIA, MOSHI
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,
Bw.William Erio, ametembelea kiwanda cha kutengeneza viatu cha Karanga mjini
Moshi mkoani Kilimanjaro Oktoba 9, 2016, ili kuona eneo ambalo kitajengwa
kiwanda kipya na cha kisasa.
Bw. Erio ambaye alifuatana na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko huo, Bw. Steven Alfred, na Meneja Uhusiano, Bi.Lulu Mengele, pia alipata fursa ya kupokea taarifa ya uendeshaji wa kiwanda cha sasa na gharama za awali za uboreshaji wa kiwanda hicho.
Bw. Erio alisema, ziara yake inalenga kujua
mambo mawili ambayo ni namna bora na ya haraka ya kuboresha kiwanda cha sasa
ili kuongeza uzalishaji wa kiwandacha sasa wakati kiwanda kipya hicho.
Pia ziara hiyo ililenga kuangalia eneo la
ujenzi wa kiwanda kipya ambacho kitakuwa cha kisasa cha kuchakata ngozi na
kutengeneza bidhaa zitokanazo na ngozi.
“Kama mtakumbuka, wiki iliyopita PPF na Jeshi la
Magereza tulisaini mkataba wa makubaliano ya kuboresha kiwanda cha sasa
na kujenga kiwanda kipya cha kisasa cha kuchakata ngozi na kutengeneza bidhaa
zitokanazo na ngozi.” Alianza kwa kusema.
Alisema, nia ya Mfuko ni kuona kazi ya ujenzi wa
kiwanda kipya inakamilika na kuanza uzalishaji kabla ya mwisho wa mwaka 2018
ili kutekeleza azma ya serikali ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa viwanda.
Aliagiza wataalamu wa PPF kwa kushirikiana na
wenzao wa Magereza (kiwanda cha Karanga), wakutane haraka ili kuainisha gharama
zinazohitajika kuboresha kiwanda cha sasa ili kuongeza uzalishaji,
Alifafanua Mkurugenzi Mkuu Bw. Erio.
Awali Kaimu Mkuu wa kiwanda cha viatu Karanga,
Naibu Mrakibu wa Magereza,( ASP), Michael Minja, alisema kiwanda cha sasa
kinakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uchakavu wa mitambo,
ambapo alisema baadhi ya mashine zimepitwa na wakati na zingine zimeharibika na
hivyo zinahitaji kufanyiwa ukarabati.
“Mambo yanayotakiwa kufanyiwa kazi ili kuwezesha
uendeshaji bora wa kiwanda, ni pamoja na kununua vipuri kwa ajili ya ukarabati
wa baadhi ya mashine, lakini pia kuna upungufu wa baadhi ya mashine hivyo
tunahitaji kuongeza idadi yake.” Alisema ASP Minja.
Akizungumza kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa
Magereza, Naibu Kamishna wa Magereza, (DCP), Editha Malya, alisema, Jeshi la
Magereza limefurahishwa na hatua iliyochukuliwa na PPF katika kushirikiana
katika uendeshaji wa kiwanda cha viatu Karanga ikiwa ni pamoja na ujenzi wa
kiwanda kipya na cha kisasa.
“Tutashirikiana kwa karibu ili kuhakikisha azma
yetu inatimia kwa haraka,” alisema DCP Malya.
Kiwanda cha viatu Karanga, kilichoko kwenye eneo
la Gereza la Karanga mjini Moshi, kilizinduliwa na Rais wa awamu ya kwanza,
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Juni 3, 1977 na wateja wakubwa wa
bidhaa za kiwanda hicho ni taasisi za kijeshi, ikiwa ni pamoja na JWTZ, JKT,
Magereza na Jeshi la Polisi.
Naibu
Kamishna wa Magereza, (DCP), Editha Malya, aliyemuwakilisha Mkuu wa
Jeshi la Magereza Nchini, (CGP), akizungumza wakati wa kikao cha kupeana
taarifa na ujumbe wa PPF ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu Erio Oktoba 9,
2016
Bw. Erio, akizungumza wakati wa mkutano huo mfupi kabla ya kukagua maeneo hayo ya ujenzi
Mkurugenzi
wa Uwekezaji wa PPF, Steven Alfred, (katikati), akizungumza jambo
wakati wa mkutano huo. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Bi. Lulu
Mengele, na kushoto ni Naibu Kamishna wa Magereza, Editha Malya
Afisa magereza ambaye ni fundi viatu wa kiwanda cha viatu cha gereza la Karanga, akishona viatu
Bw. Erio, akiongozwa na DCP Malya, na maafisa wengine akitembelea kiwanda
Kaimu
Mkuu wa Kiwanda cha kutengeneza viatu cha Karanga, Mrakibu Msaidizi wa
Magereza, (ASP), Michael Minja, akitoa taarifa ya utendaji wa kiwanda
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. Erio, na Mkurugenzi wa Uwekezaji Bw. Alfred, wakiangalia viatu vilivyotengenezwa kiwandani hapo
Bw. Erio(kushoto), akiangalia moja ya viatu vilivyotengenezwa kiwandani hapo
Mkurugenzi
wa Uwekezaji wa PPF, Bw. Steven Alfred, akionyeshwa namna kiatu
kinavyotengenezwa, (katikati) ni mwakilishi mkuu wa ofisi ya PPF mkoani
Kilimanjaro, Bw. Jacob Cornel Sulle
Mkurugenzi
Mkuu wa PPF, Bw. Erio, na Mkurugenzi wa Uwekezaji Bw. Alfred,
wakiangalia viatu vilivyotengenezwa kiwandani hapo. Kushoto ni Mkuu wa
Gereza la Karanga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, (ACP), Hassan Bakari
Mkwiche
Mkuu
wa kitengo cha umeme wa Kiwanda cha viatu Karanga, Staff Surgent,
Aulelia Mushi, akziungumzia mahitaji ya umeme kiwandani hapo
Maafisa wa wa Jeshi la Magereza, wakisikiliza mazungumzo hayo
Picha ya Pamoja baada ya kutembelea kiwanda
Ukaguzi wa moja ya maeneo ya ujenzi wa kiwanda
Jiwe la msingi aliloweka Mwalimu Nyerere wakati wa ufunguzi wa kiwanda Juni 3, 1977
Meneja
Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele, (watatu kushoto), akiangalia moja ya
viatu vinavyotengenezwa kiwandani hapo, Kushoto ni Naibu Kamishna wa
Magereza, Editha Malya, Mwakilishi Mkuu wa PPF, Mkoani Kilimanjaro,
Jacob Cornel Sulle, Mkuu wa Magereza mkoani Kilimanjaro, (RPO), Kamishna
Msaidizi wa Magereza, Anderson Kamtera, na maafisa wengine
Bw. Erio akisalimiana na Kamishna wa Magereza, DCP Editha Malya
No comments:
Post a Comment