Ofisa Mradi wa Mpango wa Magonjwa
Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele, Oscar Kaitaba akielezea umuhimu wa
vyombo vya habari kuelimisha umma kujenga tabia ya kutumia Kingatiba ya
magonjwa ya kichocho, Minyoo ya Tumbo, Usubi Matende na Mabusha wakati
wa Warsha iliyoshirikisha wanahabari, Dar es Salaam leo. Kampeni ya
kuwapatia wananchi Tibakinga kwa wakazi takribani mil. 4 wa Jiji la Dar
es Salaam itaanza Oktoba 25 waka huu. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Meneja Mradi wa Mpango wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele, Upendo Mwingira akifafanua jambo wakati wa warsha hiyo.
Wanahabari wakiwa katika warsha hiyo
Mtangazaji wa BBC, Halima Kassim
akitafakari jambo kuhusu semina hiyo ya wanahabari kupata uelewa kuhusu
magonjwa hayo na jinsi ya kuwaelimisha wananchi kutumia Kingatiba kwa
kumeza dawa mara noja kila mwaka ili kuboresha afya
Mtaalamu Kaitaba akionesha baadhi ya dawa za Kingatiba ya magonjwa hayo
Ofisa Habari wa Mradi huo, Said
Makora akiwataka wanahabari kuwaelimiasha wananchi juu ya magonjwa hayo
na jinsi ya kupata Kingatiba kwa kuandika makala, habari, majarida na
kutumia mitandao ya kijamii kwa nia ya kuyatokomeza magonjwa hayo
kufikia mwaka 2020.
Kaitaba akionesha vifaa vinavyotumika kuwapima watu ili wapewe dawa kulingana na kimo chake.
Mwandishi wa Habari wa Nipashe, Jasmin akichangia mada wakati wa semina hiyo.
Wana habari wakipatiwa dawa za Kingatiba za magonjwa hayo
Mtangazaji wa E FM Radio akipimwa urefu ndipo apatiwe dawa
No comments:
Post a Comment