Akina dada walioshiriki katika mashindano ya urembo kwa watu
wanaoishi na ulemavu wa ngozi ama Albinos jijini Nairobi, Kenya. Tarehe
21 Oktoba 2016.Mamia walijitokeza kushuhudia
maonyesho ya urembo ya Mr na Ms Albino nchini Kenya. Kila siku Albino
wanakabiliwa na hatari ya kuuawa na viungo vyao vya mwili kuuzwa
kutokana na imani za kishirikina Afrika mashariki na Afrika kusini.Chanzo-BBC SWAHILI
Malkia mpya! Louise Lihanda,
aliyeshinda taji la urembo kwa akina dada atembea jukwani akiwa amevalia
vazi la kupendeza lililotengenezwa kwa kutumia puto. Loiuse ambaye ni
mwanafunzi, amekuwa mwanamke wa kwanza kushinda taji hilo, katika
mashindano yaliyofanyika jijini Nairobi, Kenya tarehe 21 Oktoba 2016
Wanaume walioshiriki katika
mashindano hayo wasimama jukwaani. walishiriki katika mashindano ya
urembo kwa watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi ama Albinos jijini
Nairobi, Kenya. Tarehe 21 Oktoba 2016.
Mfalme! Jairus Ongetta, ambaye amekabidhiwa taji ya uanamitindo bora kwa wanaume akiwa jukwaani na mavazi ya kupendeza.
Erick Thomas, awaongoza
wanamitindo wenzake kwenye jukwaa wakati wa mashindano ya urembo kwa
watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi. Lengo lake ni kuhakikisha kwamba
watu walio na ulemavu huo wamejivunia ngozi yao.
Msichana huyu aliduwazwa na
maonyesho hayo! Yeye ni miongoni mwa watu ambao kila siku wanakabiliwa
na hatari ya kuuawa kutokana na imani za kishirikina Afrika mashariki na
Afrika kusini.
Miraba minne! John Ngatia,
ambaye pia huwa anasakata densi, avalia sare ya mapigano ya ndondi
katika maonyesho hayo, jijini Nairobi Kenya tarehe 21 Oktoba 2016
Majaji walikuwa macho! Waliongozwa na mwanamitindo wa kimataifa Deliah Ipupa (katikati) tarehe 21Oktoba 2016.
Naomi Wafula, ajitokeza
jukwaani akiwa amevalia vazi lililotengenezwa kwa sahani za plastiki
katika mashindano ya urembo yaliyofanyika jijini Nairobi, Kenya tarehe
21 Oktoba 2016
Mamia walihudhuria maonyesho
hayo kuonyesha umoja wao na watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi katika
mgahawa wa Carnivore jijini Nairobi Kenya, tarehe 21, Oktoba 2016
Amina Makokha ajitokeza jukwaani akiwa amevalia sare ya mchezo wa raga
katika mashindano ya urembo yaliyofanyika jijini Nairobi, Kenya tarehe
21 Oktoba 2016
Kutoka kulia, naibu rais wa
Kenya William Ruto, Mbunge Isaack Mwaura na mkurugenzi mkuu wa bodi ya
filamu nchini Kenya Ezekiel Mutua pia walikuwemo.
No comments:
Post a Comment