Matukio : Vijiji 24 kupata Umeme wa REA ya Awamu ya Pili mwishoni mwa Oktoba 2016, Kasulu Kigoma - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


26 Sept 2016

Matukio : Vijiji 24 kupata Umeme wa REA ya Awamu ya Pili mwishoni mwa Oktoba 2016, Kasulu Kigoma



Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wapili kulia) akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mugombe wilayani Kasulu. Kulia ni Mbunge wa Kasulu, Daniel Nsanzugwanko na kulia kwa Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Martin Mkisi.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Martin Mkisi akizungumza na wananchi wakati wa Ziara ya Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo
Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo akizungumza na wananchi. 
*************
WANANCHI wa Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma, wanataraji kuanza kufaidi umeme wa REA pindi awamu ya pili ya mradi huo itakapo kamilika mwishoni mwa  Octoba 2016.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo, alipotembelea miundombinu ya Umeme wa REA katika Wilaya ya Kasulu.

Waziri Muhongo yupo katika ziara ya siku tano mkoani Kigoma kuangalia utekelezaji wa awamu ya pili ya miradi ya REA mkoani humo na Wilayani Kasulu aliongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Kanali Martin Mkisi.

Prof Muhongo, akiambatana na Wahandisi wa Tanesco, REA na Wakandarasi wanaojenga miundombinu hiyo, wamezungumza na wananchi katika kijiji cha Mugombe na Heru Juu Wilayani Kasulu.

 Aidha katika awamu ya tatu, vijiji vipatavyo 29 vitakamilishiwa huduma hiyo muhimu kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Martin Mkisi, amewataka wananchi kutunza miundombinu ya umeme, kuchangamkia fursa za kufunga umeme wa bei rahisi na kujitokeza kwa wingi kwenye  mafunzo yatakayotolewa na Tanesco kuhusu umeme wa REA.

Pia amewaagiza wakandarasi kukamilisha usambazaji wa huduma hiyo ifikapo Octoba 30 mwaka huu bila kuongeza siku hata moja.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad