Matukio : Rais Dk. Magufuli atembelea eneo lililokuwa na Nyumba za Magomeni Kota - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Wednesday, 7 September 2016

Matukio : Rais Dk. Magufuli atembelea eneo lililokuwa na Nyumba za Magomeni Kota


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Waziri wa Ardhi Mhe John Lukuvi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe Paul Makonda, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe Ali Hapi na viongozi wengine akitembelea eneo lililokuwa Magomeni Kota jijini Dar es salaam  Septemba 6, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mwenyekiti wa waliokuwa wakaazi wa  nyumba za Magomeni Kota  Bw. George Abdi wakati alipotembelea na kuongea na wakaazi hao wa  Magomeni Kota jijini Dar es salaam Septemba 6, 2016.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Magufuli akimwagiza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Nehemia Mchechu kuendelea kuwatoa wapamgaji wenye madeni sugu kwenye nyumba ya shirika hilo wakati  alipotembelea na kuongea na wakaazi wa  Magomeni Kota wilaya ya Kinondoni  jijini Dar es salaam Septemba 6, 2016.
 Wananchi wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na mwenyekiti wa waliokuwa wakaazi  wa  nyumba za Magomeni Kota  Bw. George Abdi wakati alipotembelea na kuongea na wakaazi hao wa  Magomeni Kota jijini Dar es salaam Septemba 6, 2016.
 Kiongozi wa wakazi wa  nyumba za Magomeni Kota Bi Mwajuma  Sama akiongea machache na kuomba dua  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli   alipotembelea na kuongea na wakaazi hao wa  Magomeni Kota jijini Dar es salaam Septemba 6, 2016.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  akimfariji  Bi. Mwajuma  Sama  kwa taabu walizopata  yeye kiongozi na wakaazi wenzie  wa   Magomeni Kota jijini Dar es salaam Septemba 6, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli   akimshukuru wakili Twaha Taslima wa Law Chambers kwa kusimamia vyema maswala ya mgogoro wa eneo iliyokuwa  Magomeni Kota jijini Dar es salaam Septemba 6, 2016. PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment