Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza katika hafla
ya uzinduzi wa Kituo cha kutolea huduma "Premier Club" pamoja na Kadi ya
Kimataifa ya TemboCardVisa Infinite uliofanyika katika hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay akizungumza wakati
wa uzinduzi wa TemboCard Visa Infinite pamoja na uzinduzi wa Kituo cha
Huduma kwa Wateja Wakubwa cha Premier Club.
Naibu Spika Dk. Tulia Ackson akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo.
Naibu Spika Dk. Tulia Ackson akipeana mkono na Dk. Kimei.
Naibu Spika Dk. Tulia Ackson akipeana mkono na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Ally Laay.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza katika hafla hiyo.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay (kulia), akimkabidhi
Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson kadi ya kimataifa ya ‘TembocardVisa
Infinite’, wakati wa uzinduzi wa kadi hiyo uliokwenda sambamba na kituo
cha kutolea huduma ‘Premier Club’ jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa
wiki.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimkabidhi Kadi ya
TemboCard Visa Infinite Naibu Spika Dk. Tulia Ackson.
Naibu
Spika Dk. Tulia Ackson (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa Benki hiyo, Ally Laay (wa tatu kushoto).
Baadhi ya wageni waalikwa.
Baadhi ya wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
Wageni waalikwa wakishuhudia uzinduzi huo.
Katibu wa Benki ya CRDB John Rugambwa akiwa katika uzindui huo.
Meza Kuu.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
Wageni waalikwa.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (kulia), akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay.
Kutoka
kushoto ni Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, Mkuugenzi wa Masoko Utafiti
na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa na Mkuu wa Wilaya
ya Iringa mjini, Richard Kasesela wakicheza Kwaito wakati wa hafla hiyo.
NA ZAWADI CHOGOGWE
BENKI
ya CRDB imezindua kituo cha kisasa kwa ajili ya kuhudumia wateja
wakubwa kijulikanacho Premier Club katika jengo la Viva Tower.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dk. Charles
Kimei alisema Benki hiyo,imeamua kuzindua huduma hiyo pamoja na kadi
maalum ya TemboCard Visa Infinite kwa ajili ya watejawa kundi hilo
ikiwa ni mkakati wa Benki hiyo kuboresha huduma kwa wateja wa kundi
hilo.
Kimei alisema lengo ni kuboresha huduma kwa wateja ili kuweza kuwahudumia vizuri zaidi.
“
CRDB Bank Premier Club ni kituo maalum ambacho Benki hiyo imekizindua
kwa ajili ya kuhudumia wateaja kundi hili maalum”alisema Dk.Kimei.
Dk.
Kimei alisema kuanzishwa kwa huduma hiyo, ya wateja maalum
kitasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha na kuboresha upatikanaji wa
huduma za Benki kwa wateja huku akiamini huduma hiyo itakua ni chachu ya
kuboresha huduma kwa wateja kwa Benki hiyo kwa ujumla.
Akiongelea
juu ya huduma zitakazotolewa katika kituo hicho cha kisasa,Kimei
wateja waliojiunga na huduma hiyo watapewa kadi maalum ijulikanayo
TemboCard Visa Infinite huku wakipewa kipaumbele katika huduma
mbalimbali pamoja na kupata nafuu ya tozo na riba katika huduma
watakazo zitumia.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya CRDB Tully Mwambapa,
alisema kadi hiyo ni kadi ya kifahari zaidi na imetengenewa kwa
teknolojia ya hali ya juu kuliko kadi zote za kimataifa za malipo
duniani.
“Naomba
kuzitaja baadhi ya tu ya huduma ambazo wateja wetu wataweza kupata
kupitia huduma kupitia kadi hii ya TemboCardVisa Infinite
watejawatapewa bima ya safari pamoja na familia zao endapo watafanya
malipo kupitia kadi.”alisema Mwambapa.
Naye
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay ambaye
alikuwa mgeni rasmi alisema, Benki ya CRDB ilikuwa ya kwanza kuingiza
sokoni kadi ya malipo yaani "TemboCard" ambayo kwa kiasi kikubwa
imesaidia kuwapa wateja uhuru wa kupata huduma kwa muda na mahali
wanapotaka.
"TemboCard
iliendelea kupata umaarufu zaidi pale ilipoongeza huduma ya kuweza
kutumika nje ya nchi, au kupitia ATM za mabenki mengine, baada ya
kuungana na makampuni makubwa yanayotoa huduma za kadi ya Visa,
MasterCard na China Union na hivyo kuunda TemboCardVisa. TemboCard,
MasterCard na hivi karibuni TemboCard China Union Pay" alisema Ndugu
Laay.
Aidha
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB alisema Bodi ya
Wakurugenzi wa Benki ya CRDB ina jukumu la kuweka mazingita bora ya
uzalishaji yatakayosaidia menejimentina wafanyakazi kufikia malengo ya
kibiashara huku wakiweka mahitaji ya wateja mbele zaidi.
"
Bodi inathamini na kutoa kipaumbele utumiaji wa teknolojia na ubunifu
wa wafanyakazi wake ili kuboresha na kurahisisha huduma zake kwa wateja
na hii ndio nguzo ya pekee ambayo imeifikisha Benki yetu katika
mafanikio haya makubwa ambapo leo hii tunazindua huduma hizi za
"TemboCardVisa-Infinite" na kituo cha kisasa cha huduma kwa wateja wa
Premier yaani "CRDB Bank Premier Club" alisema Ndugu Ally Laay.
Akiongea
katika hafla hiyo, Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson
aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuzindua huduma hizo za Premier Club na
TemboCardVisa Infinite pamoja na mafanikio ambayo benki hiyo imeyapata
na kuendelea kuyapata ambayo yana akisi sera ya serikali na adhma ya
Bunge ya kutaka kujuimuisha wananchi wengi zaidi katika mfumo halali wa
fedha.
"Mimi
nikiwa kama kiongozi wa Bunge ambalo ni muhimili wa mkubwa wa nchi yet,
nimekuwa nikifarijika sana kwa namna ambayo benki yetu ya CRDB
imeendelea kukua na kuimarika na hivyo kuonyesha kuwa hata sisi
watanzania wenyewe tunaweza "Tunawapongezeni na Hongereni sana" alisema
Dk. Tulia.
No comments:
Post a Comment